Habari na Matukio

Tarehe: 14/11/2019

MAAFALI YA 24 YA CHUO CHA UANDISHI WA HABARI DAR ES SALAAM(DSJ) TAREHE 13 DESEMBA 2019Na Mwandishi Wetu

Waandishi wa habari kote nchini wakumbushwa kuzingatia misingi ya kazi ya uandishi wa habari kwa kuandika habari zenye kuchochea maendeleo ya nchi kama vile uchumi wa viwanda lakini pia Uzalendo kwa nchi yetu.


Kauli hiyo imetolewa na Naibu waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Juliana D.Shonza katika mahafali ya 24 ya chuo cha Uandishi wa Habari Dar Es Salaam(DSJ) ambapo wahitimu 346 katika ngazi Astashahada na Stashahada walitunukiwa vyeti.
Aidha Naibu waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza katika hotuba yake aliwakumbusha wanahabari kote nchini kuwa,Serikali imepitisha sheria namba 12 ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 ambayo inamtaka kila mwandishi wa habari awe na elimu ya angalau stashahada ifikapo mwaka 2021.

Hivyo kwa wahitimu wa Astashahada kote nchini ni vyema wakajipanga mapema kukidhi vigezo hivi,kwani lengo la sheria hii ni kuipa heshima tasnia hii ua uandishi wa habari na kuwaongezea thamani waandishi wa habari hapa nchini.


Naye Kaimu Mkuu wa chuo cha DSJ ndugu Seleman Shekonga kwa niaba ya wafanyakazi na wahitimu wa chuo cha Uandishi wa Habari Dar Es Salaam alimshukuru Naibu waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza kwanza kwa kukubali kuwa mgeni rasmi katika mahafali ya 24 ya DSJ,lakini pia kwa hutuba yake nzuri yenye chachu ya kuleta maendeleo katika tasnia ya habari.

“Uwajibikaji katika masomo na uzalendo ndiyo njia pekee ya kukufikisha hatika hatua ya maendeleo zaidi” hii ndiyo kauli yake kaimu Mkuu wa chuo cha DSJ ndugu Shekonga kwa wahitimu akiwataka wawe mabalozi wema huko waendako kwa kufanya kazi zao za Uandishi kwa weledi na kwa kuzingatia sheria za uandishi wa habari kama inavyoelekezwa na serikali yetu ya jamhuri ya muungano ya Tanzania.

Pamoja na chuo cha Uandishi wa Habari Dar Es Salaam(DSJ) kutoa mafunzo yake kwa njia vitendo husuani katika fani ya Televisheni,Radio pamoja na Utayarishaji wa gazeti bado chuo hiki kimepanua wigo wa kutumia sanaa kama njia mojawapo ya kuelimisha umma kwa njia ya buruduni.


Katika kuonyesha umma,kwamba vijana wa DSJ hawapo nyuma katika fani ya Sanaa baadhi ya vijana walitoka burudani mbele ya mgeni wa heshima ikiwemo michezo ya Sarakasi,dansi pamoja na kuimba hii ikionyesha kwamba wapo tayari kukabiliana na soko la ajira wakiamini kwamba sanaa ni kazi.
Aidha,katika kuunga mkono jitihada zinazofanywa na DSJ,Katibu Mtendaji wa BASATA,Godfrey Mngereza ameahidi kutoa usajili kwa baadhi ya wanachuo wahitimu waliofanya vizuri katika fani ya sanaa.
Copyright © 2021. All Rights Reserved.