Habari na Matukio

Tarehe: 30/01/2020

WABUNIFU WA MAVAZI WAHIMIZWA KUFANYA KAZI KWA WELEDI ZAIDI KAMA NJIA MOJAWAPO YA KUKIDHI MAHITAJI YA SOKO NDANI NA NJE YA TANZANIANa Mwandishi Wetu

Rai hiyo imetolewa na mbunifu wa mavazi nchini Tanzania Kulwa Mkwandule katika usiku wa MS Mkwandele’son Unforgettable Night uliofanyika katika ukumbi wa Hyatt jijini Dar Es Salaam.


Lengo la halfa hii ilikuwa ni kwa ajili ya kutoa shukurani kwa wadau wake kwa kumuunga mkono katika kazi yake ya ubunifu wa mavazi katika kipindi chote cha miaka mitanao tangu alipoanza fani hii mwaka 2015 baada ya kusajiliwa na Baraza la Sanaa la Taifa(BASATA)
Aidha Mkwandule alitumia fursa hiyo kuwashauri wabunifu wenzake kuwa kitu kimoja katika kubadilishana mawazo na ujuzi hususan fani ya ubunifu wa mavazi kwani anaamini kuwa ndiyo njia pekee ya kuitangaza fani hii kitaifa na kimataifa lakini pia kutafuta masoko kupitia majukwaa mbali mbali ya maonesho kama vile sabasaba nk.


Kazi ambazo Mkwandule amekuwa anashughulika nazo ni pamoja na bidhaa ya mavazi ya vitenge,Mabegi ya nguo,heleni nk ambapo zilioneshwa mbele ya wageni waalikwa kupitia baadhi ya wanamitindo.
Hata hivyo Mkwandule amebainisha kuwa Safari yake ya ubunifu wa mavazi katika kipindi cha miaka mitano haikuwa kazi rahisi kama hasingeshirikiana na wanadu wengine wa sanaa hii ya uunifu hapa nchini kama asingeweza kushirikiana na Baraza la Sanaa la Taifa(BASATA) kwani pale alipohitaji msaada kwao hasa nini kifanyike katika kuboresha kazi yake waliweza kumsaidia
Copyright © 2021. All Rights Reserved.