Habari na Matukio

Tarehe: 17/09/2019

UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2019Katika maohojiano na waandishi wa Habari jijini Dar Es Salaam,Katibu Mtendaji wa BASATA,aliendelea kusisitiza kuwa wasanii wana jukumu kubwa katika taifa hili kutumia vyema vipaji vyao vya sanaa kwa kupitia Muziki,sanaa za maonyesho,michoro kama njia mojawapo ya kuelimisha jamii kuhusiana na umuhimu wa chaguzi wa Serikali za Mitaa 2019 huku wao wakiwa mstari wa mbele katika kujitokeza kwenye uchaguzi huo. Ifahamike kuwa Wasanii nao ni wakazi wa mitaa mbalimbali na ni kioo cha jamii, hivyo kupewa jukumu la kuhamasisha na kuhimiza jamii zinazowazunguka ni wajibu wao na kwa kufanya hivyo kutasaidia wananchi waweze kuchagua viongozi bora katika ngazi za serikali za mtaa 2019. Uchaguzi wa Serikali za mitaa unatarajiwa kufanyika Novemba 24,2019

Copyright © 2021. All Rights Reserved.