Historia

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ni Shirika la umma lililoundwa kwa Sheria ya Bunge Na. 23 ya Mwaka 1984.Historia inaonyesha kuwa, Sheria ya kuunda upya Baraza hili ilifanywa kwa kuunganishwa Sheria ya Baraza la Sanaa la Taifa ya Mwaka 1974 na Baraza la Muziki la Taifa (BAMUTA) ya Mwaka 1974. Baraza liliundwa ili lisimamie maendeleo ya sanaa nchini


Kazi za Baraza

Kwa mujibu wa Sheria Na. 23 ya mwaka 1984, ambayo kwayo Baraza liliundwa, Majukumu ya Baraza ni pamoja na :

 • Kufufua na kuhimiza maendeleo ya kazi za Sanaa
 • Kufanya tafiti wa masuala mbalimbali ya sanaa
 • Kutoa ushauri na misaada ya kitaalamu kwa asasi au watu wanaojihusisha na shughuli za sanaa.
 • Kuratibu shughuli za sanaa zinazofanywa na watu au taasisi mbalimbali
 • Kutoa na kuimarisha mipango ya mafunzo kwa wadau wa sanaa
 • Kuishauri Serikali juu ya mambo yahusuyo maendeleo na uzalishaji wa kazi za sanaa.
 • Kuhamasisha maendeleo ya sanaa kwa njia ya maonyesho, mashindano, matamasha, warsha na semina.
 • Kuanzisha, kukusanya na kuhifadhi torwi, ikiwa pamoja na zile zinazohusu watu, asasi, taasisi, vifaa na miundo mbinu inazohusiana na sanaa
 • Kusajili wasanii na wale wote wanaojihusisha na shughuli za sanaa


Muundo wa Baraza

Baraza la Sanaa la Taifa lina wajumbe wa Baraza ambao huteuliwa na Waziri anayehusika na masuala ya sanaa. Mwenyekiti wa Baraza huteuliwa na Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mwenyekiti pamoja na wajumbe wa Baraza huteuliwa kwa kipindi cha miaka mitatu. Wakati ambapo vipindi vya kuteuliwa kwa wajumbe havina ukomo, uteuzi wa Mwenyekiti wa Baraza ni kwa vipindi viwili tu vinavyofuatana. Kwa kawaida wajumbe wa Baraza huteuliwa kwa msingi wa uwakilishi wa mikoa, asasi, asasi zinazofundisha sanaa, idara za serikali na asasi zisizo za serikali.


Baraza linaongozwa na Katibu Mtendaji, ambaye ndiye Afisa mtendaji mkuu. Baraza lina idara nne zifuatazo:

 • Idara ya fedha na utawala, inayohusika na huduma za uongozi, utumishi, uhasibu, manunuzi na usimamizi wa mali
 • Idara ya Utafiti, Habari na Mafunzo, inayohusika na shughuli za utafiti, ukusanyaji wa habari, utunzaji na usambazaji wa nyaraka pamoja na shughuli za mafunzo
 • Idara ya Uhamasishaji Mapato na Rasilimali, inayohusika na uimarishaji wa uwezo wa kifedha wa Baraza na ufadhili wa miradi ya wasanii
 • Idara ya Ukuzaji Sanaa, inayohusika na udhibiti wa ubora wa sanaa, uandaaji wa shughuli mbalimbali na ukuzaji na utangazaji wa masoko


Licha ya idara hizo tatu, kuna vitengo vitatu ambavyo hufanya kazi moja kwa moja chini ya Katibu Mtendaji. Vitengo hivyo ni vya Mipango, Sheria na cha Ukaguzi wa Hesabu wa ndani.

 • Watumishi wa Baraza
 • Wajumbe wa Baraza

Sanaa hujumuisha
 • Muziki
 • Ambao unaweza kuwa wa kuimba na wa vyombo uliorekodiwa kwa sauti au utunzi wa muziki ulioandikwa, bendi, muziki wa jazi, ala, uliorekodiwa, video, taarabu, kwaya, gwaride,muziki wa asili wa ngoma na unaoambatana na maigizo na thamthiliya.

 • Sanaa za Ufundi
 • Hujumuisha picha za kuchorwa kwa rangi, uchoraji wa kawaida, michoro ya majalada, vitabu au magazeti, uchoraji wa kwenye vitu vigumu kama metali au mbao, uandishi wa herufi ulionakishiwa, sanaa za vikaragosi kwa kutumia kompyuta na michoro iliyochapishwa. Ramani, michoro ya majengo na vielelezo, sanaa za kuumba na kuchonga, picha mgando za kamera, Kazi za usanifu majengo katika maumbo Sanaa za viwandani ikiwa pamoja na zilizo katika picha au zilizofumwa na urembo, na ubunifu wa mavazi, ususi na useketaji wa nguo.

 • Sanaa za Maonyesho
 • Michezo ya kuigiza ya jukwaani, maigizo bubu, usanifu wa majukwaa, maleba, mapambo, uandishi wa tamthiliya, ngoma na ubunifu wake, sauti na vifaa vya jukwaani, sarakasi za binadamu au za wanyama, michezo ya redio.

Copyright © 2019. All Rights Reserved.