Habari na Matukio

Tarehe: 24/10/2019

ATHARI ZA MAUDHUI YA KAZI ZA SANAA ZISIZOZINGATIA UTU WA MWANAMKE NA MAKUZI YA WATOTONa Mwandishi Wetu

Utafiti uliofanywa na plan international 2018-2019 unaonyesha kwamba wanawake ndio waathirika wakubwa wa kazi za sanaa hususani katika fani ya Sanaa ya filamu.


Inaonekana kwamba katika filamu 58 zilizofanyiwa utafiti kote duniani zinaonyesha kutwezwa kwa utu wa mwanamke(uzalilishaji wa utu wake)


Utafiti uliofanywa na nchini Tanzania kupitia Asasi isiyokuwa ya kiserikali(Bright Jamii Initiative) umebaini kuwa kwa kiasi kikubwa kuna athari za kimaadili kwa watoto wote hasa kupitia fani fani ya Muziki.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bright Jamii Initiative (BJI) Irene Fugara anasema katika mahojiano waliofanya na wazizi hapa nchini inaonyesha kwamba asilimia 85 wazazi ya wazazi hao wanasema maudhui yasiyo na maadili bora kwa watoto na kuonyeshwa katika baadhi ya vipindi vya Luninga pamoja mitandao ya kijamii yasiyo rafiki kwa wazazi na watoto kwa kutizama wakiwa pamoja na watoto kama familia.


Asilimia 50 ya Watoto waliohojiwa na Bright Jamii Initiative ,wanasema kupitia sanaa ya muziki wao wanaona ni wakawaida hata kama kama sanaa hiyo ya Muziki au filamu wasanii hao wanaonyesha maudhui yenye viashiria vya ulevi,matumizi ya madawa ya kulevya,kujihusisha na vitendo vya ngono nk na hivyo kuwashawishi kuiga tabia pamoja matendo yanayoonyesha katika kazi zao za Sanaa.


Kwa Upande wa BASATA kama wasimamizi wakuu wa kazi za Sanaa hapa nchini wanasema kuwa wasanii kama wazalishaji wa kazi za sanaa wanajukumu kuzingatia kanuni na sheria zilizowekwa na nchi yetu kama kweli wamedhamilia kuingia katika fani hii ya Sanaa ya Muziki.


Akiojiwa na Shirika la utangazaji la idhaa ya Kiswahili Ujerumani DW Katibu Mtendaji wa BASATA,Godfrey Mngereza amesema kwa kuzingatia jukumu la baraza hilo la "kusimamia, kuendeleza na kukuza kazi za wasanii na sekta ya sanaa nchini,litaendelea kutoa elimu kwa wasanii wetu ili kuzalisha sanaa iliyo bora kwa jamii na kwamba Sanaa ni Kazi na njia pekee ya kuboresha kazi zao ni pamoja na kuzalishaji wa kazi zenye Maudhui bora kwa jamii.


Mkurugenzi Mtendaji wa BJI, Irene Fugara-anashauri waandaji wa kazi za sanaa ya Muziki na Filamu kuzigatia usawa wa kijinsia kupitia mahudhui pamoja na wahusika wa kazi zao.lakini pia kwa upande wa wazazi wawe na jukumu la kufuatilia na kuelewa juu ya vipindi(program) za luninga,Radio pamoja na Mitandao ya kijamii ambavyo watoto wao wanapendelea kutizama ili waweze kudhibiti matumizi ya vyombo hivyo.


Na kwa vyombo vya habari na makampuni ya ving’amuzi, Irene amesisitiza kuzingatika kanuni zilizowekwa na mamlaka ya Mawasiliano TANZANIA zinazowataka kuahikikisha kwamba Maudhui yanayorushwa kupitia vyombo vya mawasiliano havichangii kwanza,kutweze utu wa mwanamke,kuibua hisia za ngono kwa watoto wala kuchochea tabia zozote zitakazopelekea kumomonyoka maadili kwa watoto na jamii kwa ujumla.


Copyright © 2021. All Rights Reserved.