Habari na Matukio

Tarehe: 19/10/2019

TAMASHA LA 38 LA KIMATAIFA LA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYO 19/10/2019

Na Mwandishi Wetu

Waziri wa Habari,Utamaduni Sanaa na michezo Dkt.Harrison Mwakyembe amesema kuwa ufundishwaji wa lugha ya Sanaa ni lazima uende sambamba na ufundishwaji wa lugha ya Kiswahili.
Ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa tamasha la 38 la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni mjini Bagamoyo(TASUBA) jumamosi huku kauli mbiu ya Tamasha la mwaka huu 2019 likiwa na kauli mbiu ya “Sanaa na Utamaduni Ajira Yangu” Tamasha hili linaloshirikisha vikundi mbali mbali kutoka ndani na nje ya Tanzania katika fani za ngoma,warsha,maigizo pamoja sanaa za Ubunifu,Sarakasi litakuwa la wiki moja katika Taasisi ya chuo cha Sanaa Bagamoyo.


Mwakyembe ameeleza kuwa tayari wizara yake imekwisha elekeza bodi ya wakurugenzi wa chuo hicho ianze kufikiria kuunda idara ya Kiswahili ili lugha hiyo ifundishwe rasmi. “Sanaa na lugha haviachani na ndiyo maana nimeagiza Tamasha la mwaka kesho 2020 lazima kuwe na mada itakayozungumzia lugha ya Kiswahili,alisema” Dkt.Mwakyembe Aidha Waziri Mwakyembe alitoa wito kwa wasanii wa fani ya filamu na Muziki hapa nchini kujiendeleza kimasomo ikiwa ni pamoja na kujiunga na Taasisi ya chuo cha Sanaa Bagamoyo(TaSUba) kama njia moja wapo ya kuboresha kazi zao za sanaa na kusisitiza kwamba Sanaa ni ajira lakini inakuwa ajira pindi mtu anakuwa na weledi wa kutosha hasa pale kazi ya sanaa inapokuwa na ushindani sana Sokoni.


Copyright © 2021. All Rights Reserved.