Habari na Matukio

PRESS RELEASE

Tarehe: 05/06/2020

BODI YA BASATA YAKUTANA NA WADAU WA SANAA
Na Mwandishi Wetu:

BODI ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), imepokea maoni ya wasaniii na wadau wa sanaa juu ya namna bora ya ufanyaji kazi katika kipindi hiki cha ugonjwa Covid-19, maoni haya yamepokelewa baada ya kukaa muda mrefu bila kufanya shughuli zao.


Akizungumza na wasanii katika mkutano maalum uliofanyika kwenye ukumbi wa Sanaa ulioko BASATA, Ilala jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Habbi Gunze, anasema kazi ya Baraza ni kukusanya maoni na mapendekezo na kisha kuyawasilisha Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa lengo la kupata muongozo rasmi utakaoruhusu kuendelea kutekeleza majukumu ya sanaa.


“Tunawashukuru wasanii kwa kutunga nyimbo za kupiga vita virusi vya corona na matumizi ya kuvaa barakoa, tunawaomba msubiri tamko la serikali,” alisema.


Katibu Mtendaji wa BASATA, Godfrey Mngereza, anasema wameyapokea maoni ya wadau na kueleza kwamba, athari ya corona haijamkumba mtu mmoja na kuna wa kumnyooshea mwenzake vidole kuhusu janga hilo.


Kwa upande wake, rais wa shirikisho la Sanaa za Ufundi (TAFCA), Adrian Nyangamalle, amepogeza hatua ya BASATA kukutana na wasani na wadau kupokea maoni yao ili kutengeneza muongozo wenye tija kwa wasanii.


Nyangamale, ametumia fursa hiyo kuiomba serikali kuzihamasisha taasisi zake na mashirika ya umma, kununua na kuzijali sanaa za ndani kama picha za ukutani na nyingine za ubunifu, kwani sasa hivi wateja wa nje ya nchi hawaji nchini kwa sababu ya janga la corona.


Katika kikao hicho kilichochukua saa nne, viongozi na wawakilishi kutoka vyama na mashirikisho mbalimbali ya wasanii walitoa maoni yao ya namna gani ya kuendelea na shughuli hizo wakiwemo washehereshaji,wapishi na wapambaji wa sherehe.


Katika maoni yao rais wa shirikisho la Sanaa za Maonesho, William Chitanda, amesema ipo haja ya utaratibu katika matukio yanayokuwepo kwenye sherehe za harusi kubadilishwa. Utaratibu huo ni pamoja na kupunguza idadi ya wahudhuriaji ukumbini, wahudhuriaji kuvaa barakoa na zawadi kutolewa nje ya ukumbi ili kuepuka watu kugusana mikono.


Kwa upande wao chama cha wamiliki wa Bar na kumbi za burudani, kupitia Katibu wao Potipoti Ndanga, amesema wao tayari wameanza kuchukua hatua ikiwemo kupunguza idadi ya viti na meza kwenye kumbi na bar zao.


"Wasanii ili wafanye matamasha yao wanategemea kumbi zetu za burudani, hivyo lazima na sisi tuwatengenezee mazingira mazuri ya wao kufanya kazi na wateja wao hivyo tayari tumeshaanza kuchukua hatua ikiwemo hiyo ya kupunguza idadi ya viti, meza na watu wakuingia katika kumbi zetu," amesema Ndanga.


Katibu wa Chama cha Wasanii wa Muziki wa Kizazi kipya (Tuma), Samuel Mbwana ‘Braton’, amesema kuna haja serikali kuangalia namna wasanii wataweza kupata malipo ya mirabaha kutokana na kazi zao zao ili fedha hizo ziwasaidie kujikimu katika kipindi hiki cha corona kwa kuwa kipato chao kinategemea kufanyika kwa shoo ambazo kwa sasa hazipo.


Pia amevipongeza na kuviomba vyombo mbalimbali vya habari kuendelea kufanya shoo kupitia mitandao ambazo zimeonekana kuwa mwokozi wa kupata chochote kitu kwa wasanii baada ya matamasha kusitishwa.


Mike Sangu ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya Mpito wa shirikisho la filamu, amesema kwa sasa katika uandaaji wa filamu na tamthiliya ni vyema idadi ya wanaoenda kurekodi kazi 'Location' ikapungua waende wanaorekodi tu katika eneo husika ili kupunguza idadi ya watu katika eneo husika bila kubanana.


Asha Baraka ambaye ni mmiliki wa bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’, ambaye amesema kila mwimbaji atapaswa kuwa na kipaza sauti chake.


"Katika maonesho waimbaji wamekuwa wakipokezana vipaza sauti,ni wakati sasa wamiliki wa bendi tukalisimamia hili kila msanii kuwa na kipaza sauti chake au kuwa na mifuniko ya vipaza sauti kwa kila mmoja, na pia bendi kutumia zaidi maeneo ya wazi ilikuwapa nafasi ya kutosha wadau kupata burudani ili kuwalinda na kujilinda wenyewe na maambukizi," amesema.


na wadau kupokea maoni yao ili kutengeneza muongozo wenye tija kwa wasanii.


"SANAA NI KAZI TUIKUZE, TUILINDE NA KUITHAMINI"Copyright © 2021. All Rights Reserved.