Habari na Matukio

Tarehe: 03/03/2020

MAKALA

INNOCENT MATHEWNa Mwandishi Wetu

Innocent Mathew ni Kijana aliyebobea katika mchezo wa Sarakasi hususani kamba(straps).Alizaliwa tarehe 26/03/1987 jijini Dar Es Salaam na kupata elimu yake ya msingi katika shule ya Makumbusho na baadaye elimu yake ya Sekondari katika shule ya Tegete jijini Dar Es Salaam.


Innocent anasema alianza kuupenda mchezo wa Sarakasi akiwa na umri wa miaka mitano na alipofikisha miaka kumi na moja yeye pamoja na watoto wenzake mwaka 2000 waliunda kikundi cha watu sita kikijulikana kama Black ninjar ambapo walikuwa wanakutana na kufanya mazoezi yao katika maeneo ya Mwinjuma-Mwananyamala.
Mwaka 2002 waliamua kubadilisha jina la kikundi baada ya kuchukuliwa na Wakorea na kujiita Zion Acrobatic.Ilipofikia mwaka 2003 kikundi chao kilikwenda nchini Korea kwa muda wa miezi mitatu lengo likiwa na kueneza injili kwa kupitia mchezo wa Sarakasi na baada ya hapo kikundi chao kilipata umaarufu mkubwa ndani na nje ya Tanzania na hapo ndipo likaanzishwa kundi jipya la mchezo wa Sarakasi lililojulikana kama Mama Afrika.
Kupitia mchezo huu wa Sarakasi Innocent amepata faida nyingi ikiwa ni pamoja kushiriki katika matamasha mbali mbali ya nje kama vile nchini Dubai,Martinique-Amerika ya Kusini,lakini pia amewahi kupata tuzo ya mchezaji bora wa Sarakasi nchini Dubai.
Innocent anashauri Serikali iwekeze zaidi katika mchezo huu wa Sarakasi hapa nchini kama vile kujenga kumbi za maonesho lakini kuweka matangazo katika vyombo vyetu vya Usafari zikiwemo ndege zetu za Air Tanzania,kwani kwa kufanya hivyo kutasaidia kuutangaza vizuri mchezo huu kwa wageni wanaotembelea nchi yetu.
Ifahamike kuwa Tanzania ina Utamaduni wake ikiwemo mchezo wa Sarakasi,hivyo kuna umuhimu wa kuupeleka mchezo huu katika shule za msingi ambako anaamini kuna vijana wengi ambao wanaweza kunufaika nao na hatimaye kuwapatia ajira mara wamalizapo masomo yao.


Kwa hivi sasa Msanii huyo yupo nyumbani(Tanzania) ambapo anatumia muda wake kuendesha mafunzo kwa vikundi mbali mbali vya mitaani pamoja taasisi zikiwemo shule za msingi pamoja na vituo vya watoto yatima.
Copyright © 2021. All Rights Reserved.