Habari na Matukio

Tarehe: 21/09/2019

MAPOKEZI YA WAGENI WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI KWA AJILI YA TAMASHA LA JAMAFEST 2019 JIJINI DAR ES SALAA-TANZANIA.
Na Mwandishi Wetu

Tamasha hilo ambalo linafanyika kila baada ya miaka miwili, limeshafanyika mara tatu katika nchi wanachama na mwaka huu (2019) ni zamu ya Tanzania, na litazinduliwa rasmi hapo kesho tarehe 22 Septemba 2019, ambapo Makamu wa Rais Mh. Samia Suluhu anatarajiwa kuwa mgeni rasmi. Uzinduzi huo utasindikizwa na ngoma za asili pamoja na wanamuziki wa hapa nyumbani akiwemo Diamond Platnumz, Vanessa Mdee na Barnaba. Mh. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harisson Mwakyembe akishirikiana na Naibu wake Mh. Juliana Shonza pamoja na viongozi wengine wa serikali, kwa pamoja wamewapokea wageni hao kutoka nchi tano zinazoshiriki katika tamasha hili la kiutamaduni pamoja na viongozi mbalimbali kutoka Jumuiya ya Afrika mashariki.
Dkt. Mwakyembe amewaasa Watanzania kufika kwa wingi uwanja wa Taifa kusherekea ushindi wa utamaduni wetu kwa kuwa sisi ni wamoja na pia hii ni fursa ya kuimarisha lugha yetu adhimu ya Kiswahili kwa kuwa lugha rasmi ya mawasiliano inayotumika kwenye tamasha hili ni Kiswahili
Mapokezi hayo yalipambwa na ngoma za asili kutoka nchi wanachama kutoka Tanzania Bara na Visiwani, Burundi, Kenya, Rwanda na Uganda. Nchi hizo zilionyesha umahiri mkubwa wa kucheza ngoma zao za asili na tamaduni zao.
Copyright © 2021. All Rights Reserved.