Habari na Matukio

Tarehe: 22/09/2019

JAMAFEST 2019 YAZINDULIWA RASMI JIJINI DAR ES SALAAM
Na Mwandishi WetuMakamu wa Rais amewapongeza WaziriwaHabari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh. Harrisson Mwakyembe,pamoja na Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh.Palamagamba Kabudi na Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Hamisi Kigwangala na Baraza la mawaziri la jumuiya ya Afrika Mashariki,kamati ya maandalizi pamoja na watu wote wa jumuiya ya AfrikaMashariki kwa kujituma na kushirikia kuandaa Tamasha hili la Sanaa na Kiutamaduni.
Mama Samia Suluhu amewakaribisha Wageni kutoka Nchi washiriki wa jumuiya ya Afrika Mashariki na kuwataka wajisikie wapo nyumbani,pia amewahimiza kudumisha umoja wa Nchi hizi , kutunza na kuenzi Utamaduni wetu kama waafrika.
Uzinduzi wa Tamasha hili ulisindikizwa na muziki wenye wimbo maalumu unaohusu Tamasha la Jamafest 2019 ambao umeimbwa na Msanii Peter Msechu akishirikiana na wasanii wenzake wa bongo fleva
Burudani kutoka kwa msanii diamond platnumz pamoja na Vikundi mbalimbali vya Ngoma, nyimbo na washairi kutoka nchi washiriki.
Copyright © 2021. All Rights Reserved.