Habari na Matukio

Tarehe: 24/09/2019

USAJILI WA WASANII PAMOJA NA VIKUNDI VYA SANAA KWENYE BANDA LA BASATA KATIKA MAONYESHO YA JAMAFEST 2019
Na Mwandishi Wetu

Moja ya kazi ambazo Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) inafanya katika maonyesho ya kiutamaduni ya Afrika Mashariki (Jamafest 2019) ni pamoja na kusajili na kutoa vibali na vyeti kwa wasanii na wadau wanaofika kutembelea banda letu. Bwana Jelson Enock Lyamba ni mojawapo wa msanii wa Uchoraji anayemiliki Kampuni ya Lyamba Painter kutoka Katoro Geita nchini Tanzania na pia ni mshiriki wa Tamasha la Utamaduni la Jamafest 2019 ambaye amefanikiwa kujisajili baada ya kutembelea banda la Basata na kukabidhiwa kibali halali cha kufanya kazi za Sanaa pamoja na cheti cha usajili. Faida za kutambuliwa na kusajiliwa na Basata ni pamoja na kuendesha shughuli zake za Sanaa kwa mujibu wa sheria za nchi,sambamba na kutambuliwa kwa shughuli za msanii huyu hivyo kufanya kazi kihalali.Copyright © 2021. All Rights Reserved.