Habari na Matukio

Tarehe: 25/09/2019

SANAA ZA UCHONGAJI NA UCHORAJI KUTOKA BURUNDI
Na Mwandishi Wetu

Bwana Nkurikiye Jamari alielezea kuwa sio mara yake ya kwanza kuja Tanzania kwani alishawahi kuhudhuria matamasha mengine kama vile sabasaba lakini pia akaelezea jinsi gani watanzania walivyo wakarimu kwa wageni wanapotembelea nchi hii. Bwana Nkurikiye Jamari ameendelea kueleza kuwa tamasha la jumuiya la utamaduni na Sanaa la Afrika mashariki jamafest 2019 linalofanyika nchini Tanzania ni Tamasha lililoandaliwa vizuri na limewapatia elimu ya kiufundi na mafunzo makubwa ya kuwafungua macho kutoka na na muunganiko wa watu kutoka Nchi mbalimbali kama vile Kenya, Uganda, Rwanda na wenyeji Tanzania. Sisi kama waafrika Sanaa zetu zimefanana kwa kiasi kikubwa japo kuna tofauti kidogo tu za kiufundi mfano Tanzania vikapu vyao wanatengeneza kwa ukili wakati kule Burundi vinatengenezwa kwa kutumia majani ya mahindi pia kuna viti vinazyotengezezwa kwa kutumia mti wa Mwanzi. Changamoto kubwa wanayokutana nayo ni uchache wa wateja pale ambapo wanakuja kununua bidhaa yao na hivyo kujikuta kubakiwa na bidhaa hiyo na kujikuta wakirejea nayo tena warudipo nchini kwao Burundi Kuhusu Ngoma za Burundi Bwana Nkurikiye anasema ngoma hizo za asili zinatengenezwa na miti na kuwambwa juu na ngozi ya ng’ombe na hupigwa na wanaume kwa madoido ya kucheza na kuruka huku wanawake wakiwasindikiza nyuma kwa kucheza.Copyright © 2021. All Rights Reserved.