Habari na Matukio

Tarehe: 27/09/2019

BASATA NA MSANII WA KAZI ZA MIKONO KUTOKA KENYA KWENYE TAMASHA LA KIUTAMADUNI LA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI JAMAFEST 2019
Na Mwandishi Wetu

Mary ni msanii katika kampuni ya Bombolulu Workshops and cultural center iliyopo Mombasa nchini Kenya ambayo inatengeneza bidhaa mbalimbali kama vile kushona nguo, mikoba, shanga za shingoni na kiunoni pamoja na hereni. Mary anasema ni mara yake ya kwanza kushiriki katikat amasha la jamafest ambapo kupitia Tamasha la mwaka huu amepata fursa ya kujifunza mambo mbali mbali katika fani ya sanaa na biashara. Aidha kupitia tamasha hili limempatia mwanga kwa kujionea vitu vingi vya kiutamaduni ambavyo kama kikundi wanaamini wakianza kuvitengeneza katika kampuni yao vitapata soko zuri na kuasaidia kujiendeleza kibiashara. Mjasiriamali huyu ameeleza furaha yake kuwepo nchini Tanzania kwani watu wake ni wakarimu na heshima nyingi na kuwashauri wengine ambao hawajaweza kufika katika tamasha la jamafest2019 watafute nafasi wakati mwingine kushiriki kwani kuna vitu vingi vizuri vyakujifunza kutoka nchi washirika wa Afrika mashariki na kwani kwa kufanya hivyo kutasaidia kukuza biashara miaongoni mwao na hatimaye kuinua kipatato kwa mtu mmoja moja na nchi kwa ujumla.Copyright © 2021. All Rights Reserved.