Habari na Matukio

Tarehe: 27/09/2019

JAMAFESTIVAL FASHION SHOW 2019 JIJINI DAR ES SALAAM TANZANIA
Na Mwandishi Wetu

Mojawapo ya fani zilizoonyeshwa katika Tamasha hili ni pamoja na Jamafestival Fashion Show 2019 jijini Dar Es Salaam ni pamoja na ubunifu wa Mavazi kutoka nchi shiriki kutoka Afrika ya Mashariki,walionyesha mavazi yao yaliyotengenezwa katika mitindo mbali mbali. Hii ilikuwa ni fursa pekee kwa wabunifu kutoka nchi hizi kuonyesha ubunifu wao wa kutengeneza mavazi kwa kutumia malighafi zinazopatikana katika nchi zetu hususani zao la Pamba lakini pia kutafuta masoko ndani ya nchi zetu za Afrika ya Mashariki pamoja na nchi za nje. Katika Tamasha hili la mavazi lilihudhuriwa na viongozi mbali mbali Wakiwemo Waziri na Naibu waziriki wa Wizara ya Habari,Utamaduni na Michezo Mh.Harrion Mwakyembe,Naibu wake Juliana Shonza pamoja na Mwenyekiti wa Jamafest2019 Joyce Fisso Pamoja na kuwempo maonyesho mbali mbali ya sanaa kutoka kwa wasanii wan chi tano zilizoshirika katika tamasha la Utamaduni la Afrika Mashariki yaani Tanzania,Kenya,Uganda,Rwanda na Burudi fani nyingine iliyoshiriki ni upande wa Chakula cha Asili ambapo umahiri mkubwa ulionyeshwa na washiriki katika wa chakula hususani nyama choma. Hii ilikuwa ni frusa pekee kwa wajasiliaMali kuonyesha ustadi wao katika mapishi ya asili lakini pia kama njia mojawapo ya kujipatia kipato kupitia Tamasha hili la Utamaduni kwa nchi za Afrika Mashariki.

Copyright © 2021. All Rights Reserved.