Habari na Matukio

Tarehe: 28/09/2019

KUFUNGWA RASMI KWA MATAMASHA YA JAMAFEST NA URITHI FESTIVAL 2019 JIJINI DAR ES SALAAM.
Na Mwandishi Wetu

Aliongezea kwakusema kuwa tamasha hili limekuja kupanua wigo wa mawasiliano, kuimarisha hali ya undugu na uchangamano baina ya nchi hizi, na kukuza biashara ya bidhaa za asili huku akiwataka wanajumuiya kuwa na nidhamu pamoja na kushirikiana katika mambo yote yatakayoimarisha jumuiya ya Afrika Mashariki. Pongezi nyingi pia zilikwenda kwa wa wawakilishi wanne wa jumuiya ya Afrika Mashariki walioshiriki kupanda mlima Kilimanjaro kwa muda wa siku sita na kupandisha nembo ya Jamafest 2019 na Urithi Festival ikiwa ni katika juhudi za kutangaza matamasha haya nje ya mipaka ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Dkt. Harrison Mwakyembe amewashukuru viongozi wa Serikali kwa ushirikiano walioonesha kutoka mwanzo wa tamasha hili mpaka mwisho nakueleza kuwa tamasha hili limefungua fursa pana na mpya kama vile fursa za kufahamiana, na fursa za kibiashara kwa kazi za Utamaduni na Sanaa. Na yeye Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii nchini, Mhe. Costantine Kanyasu aliwapongeza wawakilishi waliopanda mlima Kilimanjaro ambao wameonyesha uzalendo katika kuchagiza matamasha ya Jamafest na Urithi Festival na kutoa wito kwa wananchi kuendelea kujitokeza kwa wingi kwenye tamasha la Urithi Festival litakaloendelea kufanyika katika mikoa 10 ili waweze kuonyesha uasili wao katika vyakula, mavazi pamoja na ngoma zao.


Copyright © 2021. All Rights Reserved.