Habari na Matukio

Tarehe: 11/10/2019

KUMBUKIZI YA KIFO CHA BABA WA TAIFA, MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE.
Na Mwandishi Wetu

Hoteli ya jaromax palace ya jijini Dar Es Salaam Imeingia udhamini na Taasisi ya Miss Utalii Tanzania wa hali na mali unaofika thamani ya ya shillingi za kitanzania Millioni miamoja hamsini na mbili ukijumuisha huduma za malazi, chakula, vinywaji na huduma za ukumbi wa mikutano na mazoezi kwa washiriki, viongozi na waandishi wa habari katika hatua za ngazi mbalimbali za shindano hiloTanzania.
Akizungumza na waandishi wa habari Meneja wa Hotel ya jaromax palace, ndugu Thomas Fusi ameeleza kuwa uamuzi wa kudhamini shindano hili umetokana na tija na umuhimu wa shindano hili pekee Nchini la urembo wa kitalii na kiutamaduni katika kutangaza vivutio na huduma za utalii kitaifa na kimataifa kila mwaka. Aidha Mkurugenzi wa Mashindano na Matukio wa Miss Utalii Tanzania Bi.Geogina Saulo amesema kuwa Udhamini huu ni Uthibitisho wa hadhi na ubora wa nyota nne hadi tano wa hoteli na huduma za kitalii zinazo patikana katika hoteli hii kwa bei ambazo zinazingatia uwezo wa vipato vya kada zote, kukuza Utalii kwa amani na usalama wa hali ya juu uliopo katika hoteli hii,kupitia kampeni ya Miss Utalii Tanzania ya kuhamasisha Utalii wa ndani ya UTALII USWAHILINI na MISS UTALII TANZANIA ambayo itazinduliwa hivi karibuni sambamba na uzinduzi wa shindano na semina elekezi ya waratibu wa kanda na wahariri wa vyombo vya habari.
Moja ya wageni waliohudhuria katika hafala hii ni Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ambapo Kaimu Afisa Habari na Mawasiliano,Godfrey Nicolaus Nago aliwapongeza Menejimenti ya Hoteli ya Jaromax Palace kuwa wadhamini rasmi wa shindano la kimataifa la miss utalii Tanzania 2019/2020 na wenye dhima ya kikomo ya kuendesha shindano hili Nchini.


Washiriki zaidi ya 100, wenye mataji ya kitakaifa kutoka zaidi ya nchi 100 duniani watashiriki shindano la kimataifa la Miss Utalii Tanzania 2019/2020 litakalo fanyika nchini Tanzania Juni 2020. Miss Utalii Tanzania ni alama ya Urithi wa Taifa,Utalii ni maisha,Utamaduni ni Uhai wa Taifa(Miss Tourism Tanzania,the symbol of national Heritage ,Tourism is life, Culture is Living)
Copyright © 2021. All Rights Reserved.