Habari na Matukio

Tarehe: 14/02/2020

KIKAO CHA KATIBU MKUU NA WAFANYAKAZI WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO DKT. HASSAN ABBAS KATIBU MKUU NA MSEMAJI MKUU WA SERIKALINa Mwandishi Wetu

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbas amekutana na wafanyakazi wa wizara hiyo jijini Dar Es Salaam kwa ajili ya kupeana misingi itakayowasaidia wafanyakazi kwa pamoja kufikia matarajio ya Wizara ambayo pia ndiyo matarajio ya Serikali.


Katika kuweka mambo sawa ndani ya Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo, Katibu Mkuu Dkt.Abbas amesema mambo kadhaa inabidi yafanyike kwa kasi zaidi kama vile huduma ili kusukuma mbele majukumu mengi tuliyokasimiwa yaende na kutatua changamoto zilizopo kwa hivi sasa,kuwajali wafanyakazi pamoja na kutatua changamoto ya vitendeakazi ndani ya Wizara.
Aidha amewakumbusha wafanyakazi, kama kweli wanataka kufikia matarajio waliyojiwekea jambo la muhimu ni kuwa Wachapa kazi,Waadilifu na Wazalendo ndani ya Wizara na Serikali lakini pia kuwa wabunifu na kuacha kufanya kazi kwa mazoea.
Katika kuhitimisha risala yake kwa wafanyakazi wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo, Katibu Mkuu Dkt.Abbas amesisitiza kuwa, itakuwa kazi bure katika kupata maendeleo kama hatutafuata siri sita(6) za mafanikio ambazo ni pamoja na:

  • Kuweka Malengo
  • Kuweka Malengo Makubwa na Magumu
  • Mipango ya Utekelezaji na kutekeleza mikakati ya Wizara na sekta zake.
  • Mawasiliano ndani Wizara na Sekta ni muhimu. Mahali pa kazi panaweza kuwa na malalamiko na manung’uniko mengi kama wafanyakazi hawapewi MREJESHO na KWA WAKATI kuhusu mambo mbalimbali yanayohusu maslahi yao, haki zao na wajibu wao.
  • Kushirikiana. Siri zote 4 haziwezi kufanikiwa iwapo hakuna USHIRIKIANO kati ya wafanyakazi, viongozi na wafanyakazi.
  • Tumwamini na kumuomba Mungu kwa imani zote ili pale nguvu na uwezo wetu vinapoishia aweze kutuangazia kwani yako mambo tunaweza kuyatimiza sisi kama wanadamu lakini asilimia kubwa pia yapo nje ya uwezo wetu.
Katika hatua nyingine Sekretarieti ya Maadili ya Utumishi wa Umma kupitia kwa Mkuu wa Kanda Maalum ya Viongozi,Bi. Getrude Ciriacus aliendesha semina juu ya kiapo cha uadilifu na kufuatiwa na kiapo cha ahadi ya uhadilifu kwa wafanyakazi wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo mbele ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbas.
Copyright © 2021. All Rights Reserved.