Habari na Matukio

Tarehe: 10/03/2020

TAARIFA YA KIKAO MAALUMU CHA TATU CHA BODI YA BASATA KILICHOFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM.Na Mwandishi Wetu

Katika kuhakikisha Bodi ya BASATA, inapokea, kupitia na kujadili kwa kina kuhusu masuala ya mapato, matumizi ya fedha na hesabu za Baraza, kilifanyika kikao maalum cha Bodi ya BASATA tarehe 10/03/2020 katika ofisi za BASATA Ilala Shariff Shamba chini ya Mwenyekiti wa bodi hiyo, Bw.Habbi Gunze kwa lengo la kupokea na kupitia ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha wa 2018/2019.
Wajumbe wa Bodi walioshiriki katika kikao hiki ni pamoja na Katibu Mtendaji wa BASATA, Godfrey Mngereza, Dkt.Asha S. Mshana, Dkt.Emmanuel M. Ishengoma, Dkt. Sandia J. Mwakaje, Hamis M. Mtambalike pamoja na Hamis M. Mwinjuma walihudhuria kikao hiki.
Aidha katika kikao hiki Bw. Allen Kisute ambaye ni Mkaguzi wa Hesabu kutoka Kampuni ya KESTON LEVITICUS AUDIT FIRM ambayo ni Kampuni inayofanya ukaguzi wa Hesabu za Baraza kwa niaba ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),aliwasilisha ripoti hiyo kwa ufupi mbele ya Bodi. Mkaguzi huyo aliipongeza Bodi na Menejimenti kwa kuwa na idadi ndogo ya hoja za ukaguzi na kwamba kazi imefanyika kwa ufanisi,hivyo kushauri BASATA kuendelea na utekelezaji wa Majukumu yake kwa kuzingatia Sheria,Kanuni na taratibu za kusimamia maendeleo ya Sanaa Tanzania.
Copyright © 2021. All Rights Reserved.