Habari na Matukio

Tarehe: 25/01/2021

KIKAO CHA MAENDELEO YA SANAA KANDA YA KASKAZINI MWAKA 2020/2021Na Mwandishi Wetu

Washiriki wa maendeleo ya kazi za Sanaa kutoka kanda ya Kaskazini, mikoa ya (Arusha,Manyara,Kilimanjaro na Tanga) wakiwemo maafisa utamaduni wa kanda,Tamisemi,wawakilishi wa wasanii na wadau wa sanaa, tarehe 18/01/2021 hadi 22/01/2021 wanakutana jijini Arusha katika hotel ya Point zone resort,ambapo pamoja na masuala mengine mkutano huo unalenga kuimarisha mahusiano baina ya BASATA
maafisa utamaduni,wasanii na wadau wa sanaa kanda ya Kasikazini,lakini pia kuimarisha mfumo wa utendaji wa kazi za Sanaa ili kuongeza umoja na mshikamano kiutendaji kati ya Baraza la Sanaa la Taifa,maafisa utamaduni,wasanii na wadau wa sanaa kanda ya Kaskazini,na kujadili kwa pamoja mikakati ya ukuzaji sanaa na hatimaye kutengeneza mpango kazi wa maendeleo ya sanaa kanda ya kaskazini,lakini pia wadau kulijua baraza kwa undani zaidi.
Waandaaji wa mkutano huu ni BASATA chini ya waratibu Flora Mgonja na Mrisho Mrisho,kwa kushirikiana na maafisa Utamaduni wa Kanda ya Kaskazini pamoja na wadau wa Sanaa.
Mgeni rasmi katika ufunguzi wa mkutano huo alikuwa ni Mkurugenzi wa maendeleo ya michezo,Idara ya elimu(Tamisemi)Bw. Leonard Thadeo sambamba na Mkurugenzi wa makumbusho ya taifa jijini arusha Dkt.Christine Fishaa Ngereza ambaye alikutoa rai kwa washiriki wa mkutano huo, juu ya usimamizi na uhifadhi wa mila,utamaduni na utunzaji wa mazingira katika maeneo yenye vivutio vyote vya asili hapa nchini.
Copyright © 2021. All Rights Reserved.