Tarehe: 12/10/2022
Kikao mkakati cha ushirikiano kuinua sekta ya Sanaa Kati ya watendaji wa BASATA na wadau kutoka ubalozi wa Ufaransa kimefanyika Leo tarehe 12 Oktoba, 2022

Na Mwandishi Wetu
Kikao mkakati cha ushirikiano kuinua sekta ya Sanaa Kati ya watendaji wa BASATA na wadau kutoka ubalozi wa Ufaransa kimefanyika Leo tarehe 12 Oktoba, 2022 kikiongozwa na Katibu Mtendaji Dkt. Kedmon E. Mapana.
Wakati wa majadiliano, wataalam kutoka ubalozi wa Ufaransa wameonesha kupendezwa na ubunifu WA kazi mbalimbali za Sanaa zinazofanyika hapa nchini huku wakiahidi kutanua wigo wa ubunifu ili kusaidia wasanii wa Tanzania kutoa kazi zenye ushindani wa soko la ndani na nje ya nchi.
Wameendelea kusema kuwa, wakati wa utekelezaji wa Mradi wa Umoja unaowakutanisha wasanii kutoka Ulaya na Afrika Mashariki wataweza kutoa ujuzi katika fani mbalimbali ikiwemo utengenezaji wa filamu fupi ikiwemo video fupi za wanamuziki zenye kukonga nyoyo za hadhira ili waweze kulikamata soko Kwa urahisi.
Kwa Upande wake Katibu Mtendaji BASATA, amewahakikishia ushirikiano wa kutosha unaolenga kuinua sekta ya Sanaa, amewaomba ushirikiano ujikite katika kuwajengea uwezo wataalam, viongozi wa mashirikisho pamoja na wasanii hasa kwenye upande wa kuandaa maandiko na kutafuta masoko kwakuwa eneo hilo lina changamoto kubwa Sana.
Ameendelea kusema kuwa, kwa kutambua fursa watakayoipata wasanii wa Tanzania kupitia Mradi wa Umoja, BASATA imeamua kutowatoza wasanii wanaokuja kwaajili ya Mradi huo ikiamini kuwa watakuwepo kwaajili ya kuleta ujuzi na siyo kupata faida hivyo Baraza limeonesha nia ya ushirikiano tangu mwanzo.
Juu ya hapo, ugeni huo umeweza kupata taarifa ya programu mbalimbali zinazotekelezwa na BASATA ambazo kwazo wanaweza kuzichambua baadhi zitakazowapa fursa ya kuzifanyia ufadhili waweze kufanya hivyo.
Ugeni kutoka ubalozi wa Ufaransa walotembelea ofisi ya BASATA ni Bwana Patrick Cohen, Gaell Jones, Serge Nokoue na Kevin Theze.


