Habari na Matukio

Tarehe: 28/09/2019

WASANII WA PILIPILI MUSIC MANIA WAPEWA VYETI VYA USAJILI KUTOKA BASATA.
Na Mwandishi Wetu

Hayo ameyazungumza Katibu Mtendaji wa BASATA ndugu Mngereza, wakati wa kabidhiwa vyeti vya usajili kwa wanamuziki chipukizi kutoka lebo ya Pilipili Music Mania,ambao wamekamilisha usajili wao kutoka Baraza la Sanaa La Taifa .
Pilipili Music Mania ni lebo inayojishughulisha na shughuli za sanaa ya muziki, ambayo kwa sasa imekamilisha usajili wake kutoka Baraza la Sanaa la Taifa kwa kupokea vyeti ,ikiwa imesajili wasanii chipukizi wane ambao ni pamoja na Moses George (Monyati) Moasoor Rashid(Ragvox),Juma Awadhi(Bladykey)Abubakari Mrisho(Fainally).
Aidha,ndugu Godfrey Mngereza amewataka pia wasanii na wadau wote wa sanaa kufika BASATA kwa ajili ya ushauri kwa masuala yote yanayohusiana na kazi za sanaa pamoja na mikataba,pia kuiga mfano kutoka kwa Pilipili Music Mania kwa kufika BASATA ili kukamilisha usajili wao kwanza, kabla ya kujishughulisha na shughuli zozote zinahusu kazi za sanaa.


Copyright © 2021. All Rights Reserved.