Habari na Matukio

Tarehe: 23/09/2019

NCHI YA MAYOTTE YAFUNGUA KITUO KIKUBWA CHA VITABU VYA ELIMU NCHINI TANZANIA
Na Mwandishi WetuWaziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Harrison Mwakyembe ametoa wito kwa Watanzania hususani Vijana kujenga Utamaduni wakupenda kujisomea vitabu kama njia mojawapo ya kujipatia maarifa kwa ajili ya maendeleo ya taifa letu.


Rai hiyo ameitoa katika uzinduzi wa Taasisi hii ya IBAE nchini Tanzania, inayojumuisha mashirika ya kimataifa ya Vitabu vya Elimu yenye makao yake makuu nchini Mayotte barani Afrika, Aidha Mhe.Mwakyembe amewasifu Wananchi wa nchi ya Mayotte chini ya Rais wa taasisi hiyo ya INTERNATIONAL BOOK AGENCY FOR EDUCATION(IBAE) Bwana Mouhoutar Salim kwa kuichagua Tanzania kuwa kituo kikuu cha Taasisi hiyo kwa nchi washirika ambazo ni Mayotte,Tanzania,Madagascar,Comoro,Msumbiji pamoja na Kenya,na kuahidi kuwa Tanzania itakuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa malengo yote yaliyokusudiwa yanatekelezeka.
Naye Rais wa taasisi hiyo ya INTERNATIONAL BOOK AGENCY FOR EDUCATION(IBAE) Bwana Mouhoutar Salim alimshukuru Waziri Harrison Mwakyembe kwanza kama mwana taaluma na mwandishi wa Vitabu kuja kuzindua Taasisi hiyo ambayo kimsingi itatumika kuwaunganisha waandishi wa vitabu kutoka nchi hizi sita za Mayotte,Tanzania,Madagascar,Comoro,Msumbiji pamoja na Kenya katika kupromote vitabu.
Aidha Rais huyu wa IBAE,Bwana HOUHOUTAR,amesema kupitia taasisi hii waandishi wa vitabu watapata fursa ya kuunganishwa pamoja katika kufanya tafiti na kuandika mambo mbali mbali ya kijamii na elimu juu ya maendeleo ya watu wake hususani katika Nyanja za kilimo,Uvuvi, Tehama,Biashara lakini pia akaimiza watu wapende kujisomea vitabu husuani watoto kwani kwa kufanya hivyo kutasaidia kuwajengea msingi mzuri wa baadaye katika elimu yao.


Naye Mgeni rasmi katika uzinduzi wa Taasisi hiyo ya ABAE,kupitia mradi wake wa mashirika ya kimataifa ya vitabu vya Elimu, Rais Mstaafu wa Mayotte Mhe.Ahmed A. Douchina amewataka waandishi wa vitabu kwa nchi washirika kuja na mkakati maalum ambao utatumika kuchochea maendeleo ya nchi zetu hizi kupitia uandishi wa vitabu. Ifahaamike kuwa historia ya nchi hizi sita, yaani Mayotte,Tanzania,Madagascar,Comoro,Msumbiji pamoja na Kenya zinaunganishwa katika misingi ya kihistoria yaani mila,desturi na Utamaduni.
Aidha Mgeni Rais Mstaafu wa Mayotte Mhe. Ahmed A.Douchina alimkabidhi Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Harrison Mwakyembe vitenge pamoja na vitabu kutoka Mayotte kama njia mojawapo ya kudumisha ushirikiano kati ya nchi hizi mbili yaani Tanzania na Mayotte
Copyright © 2021. All Rights Reserved.