Habari na Matukio

Tarehe: 13/10/2022

Mcheza filamu na mwanamitindo wa kimataifa kutoka Uingereza Ndugu Oris Orhuero Leo tarehe 13 Oktoba, 2022


Na Mwandishi Wetu


Mcheza filamu na mwanamitindo wa kimataifa kutoka Uingereza Ndugu Oris Orhuero Leo tarehe 13 Oktoba, 2022 amewapa nafasi kubwa wasanii wa Kitanzania kushirikiana nae ili kutengeneza kazi za Sanaa zenye kuakisi mandhari na utamaduni unaotam ulisha thamani halisi ya Tanzania.


Ameyasema hayo wakati akizungumza na wasanii na wabunifu wa mitindo waliojitokeza katika ukumbi wa Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Kwa lengo la kukutana kisha kujadiliana juu ya ubunifu na soko la kazi za Sanaa kitaifa na kimataifa.


Msanii huyo ambaye ametamba na uhusika wake katika filamu ya "Sometimes in April" aliyocheza na Idris Alba, amesema kuwa nchi imebarikiwa kuwa na wasanii vijana wenye ari ya kufanya kazi hivyo wanatakiwa kufanya kazi zenye ubora wa hali ya juu huku wakizingatia hitaji la mashabiki wao Kwa wakati husika kwasababu Sanaa ni hisia, ukifanikiwa kugusa hisia za mtu ujue umefanikiwa.


Juu ya hapo, amesisitiza matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii Kwa kufanya kazi fupi kisha kuzipost kwasababu wadau wengi wanaotafuta vipaji ili wawekeze wanafuatilia Sana mitandaoni kikubwa wanatakiwa kuongozwa na ubunifu.


Kabla ya kikao hicho, Ndugu Orhuero ameeleza kufanya kikao na Katibu Mtendaji BASATA Dkt. Kedmon E. Mapana na wataalam wake ambapo Kwa pamoja wamekubaliana kushirikiana katika maeneo ya kimkakati kukuza Sanaa nchini
Copyright © 2021. All Rights Reserved.