Habari na Matukio

Tarehe: 24/08/2019

SHINDANO LA MISS TANZANIA 2019.
Na Mwandishi WetuShindano la kumsaka mlimbwende wa Tanzania yaani Miss Tanzania limefanyika usiku wa kuamkia jumamosi tarehe24 Agosti, 2019 katika ukumbi wa Kisena Millenium Tower, Dar es salaam nakuhudhuriwa na watu mbalimbali akiwemo waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe ambaye ndio alikuwa mgeni rasmi.
Shindano hilo lililoandaliwa na mkurugenzi wa kampuni ya The Look Basilla Mwanukuzi likihusisha warembo 20 waliokuwa wamejichimbia kufanya mazoezi katika hotel ya Serene iliyopo Mbezi beach, Dar es Salaam.
Washiriki hao 20 ndio waliokuwa wakiwania taji hilo lililokuwa likishikiliwa na mrembo Queenelizabeth Makune. Basilla ambaye alishawahi kuwa Miss Tanzania 1998 alisema, ‘washiriki wote ni wenye sifa na vigezo vya kuweza kutwaa taji hilo hivyo, wadau wa urembo wajiandae kushuhudia mshindi mwenye vigezo vya kufanya makubwa katika kinyang’anyiro cha dunia’’.


Waliohudhuria wengine ni aliyewahi kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu, wa wakilishi kutoka Baraza la Sanaa La Taifa (BASATA), ugeni kutoka kwa mlimbwende wa kisiwa cha Mayotte, Miss Mayotte 2018 Ousna Attouman na baadhi ya warembo waliowahi kushiriki Shindano hilo akiwemo Miriam Odemba na Nelly Kazikazi.


Usiku wa Shindano la Miss Tanzania ulimalizika kwa Chief jaji Shyrose banji kumtaja mrembo mwakilishi kutoka kanda ya ziwa yaani Mwanza, Silvia Sebastian kuwa ndiye aliyejinyakulia taji hilo huku akiwashinda washiriki wenzie 19 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania. Na ataiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Miss World yatakayo rindima jijini London Uingereza Desemba 14, 2019.


Mrembo Silvia aliondoka na kitita cha shilingi Milioni 10 huku mshindi wa pili Grayres Amosi akiondoka na sofa lenye thamani ya Shilingi Milioni 2 na mshindi wa tatu Queen Antony akiondoka na Sh.Milioni 1.
Mrembo huyo, anayeshikilia taji la Miss Tanzania 2019 amesema kuwa, ‘‘katika muda atakao kuwa anashikilia taji hilo, moja ya mambo anayotarajia kuyafanya ni utoaji wa elimu ya kodi kwakua asilimia kubwa ya watanzania bado hawajaona umuhimu wa kulipa kodi; atafanya hivyo akishirikiana na baadhi ya warembo wenzie ili kuweza kufikisha elimu hiyo kwa jamii ili wapate uelewa wakulipa kodi wenyewe bila kusukumwa’’


Copyright © 2021. All Rights Reserved.