Habari na Matukio

Tarehe: 28/08/2019

KIKAO CHA MH. WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO DK. HARRISON MWAKIYEMBE PAMOJA NA WASANII NA WADAU WA SANAA
Na Mwandishi Wetu

Waziri wa Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Dr.Harrison Mwakyembe ameongea na wasanii na wadau wa Sanaa kwenye ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Center (JNICC), kuhusiana na wazo la kuunganisha taasisi za BASATA, Chama cha Hakimiliki Tanzania (COSOTA) na BODI YA FILAMU.
Mkutano huo, lengo lake lilikuwa ni kuunganisha Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA),Bodi ya Filamu na Chama cha Haki miliki Tanzania (COSOTA) ili kuboresha na kuleta mageuzi makubwa katika sekta ya Sanaa na Ubunifu, na kusogeza huduma kwa wasanii na wabunifu.
Mbali na kujadili mchakato wa uundwaji wa mamlaka moja ya kusimamia sekta ya sanaa na Ubunifu,pia mkutano huo ulijadili juu ya magawiwo wa mirabaha kwa kazi za wasanii na muziki.


Viongozi wa mashirikisho mbalimbali ya sanaa na wasanii walipata wasaa wa kujadiliana, kisha kuwasilisha mapendekezo kuhusiana na mjadala huo.Ambapo Katibu Mkuu wa Chama cha Muziki wa Dansi Tanzania (CHAMUDATA),Hassani Msumari alisema ‘wizara na wataalamu kwa vilio vyetu vingi huko nyuma,tulikuwa tukiomba viunganishwe kuondoa ukiritimba,sasa hili la Filamu na Basata halina hoja.Ila Cosota wengi wetu,hata mimi kuunganisha hatutaki,hata sheria za dunia za haki miliki hazitaki’.ema.


‘Cosota haiwezi kuchanganywa na huo utatu ,bora tubakie na Bodi ya Filamu na BASATA’ alisema Ado Novemba Rais wa shirikisho la Muziki wa Injili (TAF).Naye Rais wa Shirikisho la Filamu nchini,Simon Mwakifamba alisema kuwa haoni haja ya kuunganisha Cosota na hizo taasisi nyingine kwa sababu wao ndio wanaopaswa kusimamia maslahi ya wasanii,japokuwa hakuna kilichofanyika hadi sasa.
Miongoni mwa wasanii nguli waliojitokeza katika mkutano ni pamoja na Mzee King Kiki, Richard Mabala na wengineo


Copyright © 2021. All Rights Reserved.