Habari na Matukio

TANGAZO KWA WASANII WOTE

Tarehe: 15/06/2015

YAH: MWALIKO WA KIKUNDI CHA SANAA KUSHIRIKI KATIKA MAONESHO YA KILA MWAKA YA ZAMBIA KUANZIA TAREHE 29 JULAI, HADI 03 AGOSTI, 2015.

Tafadhali rejea kichwa cha habari hapo juu.


Baraza la Sanaa la Taifa limepokea taarifa ya mwaliko tajwa kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kuwa Wizara ya Kilimo na chama cha Kijamii nchini Zambia imeandaa maonesho ya Sanaa yatakayofanyika kuanzia tarehe 29 Julai, hadi 03 Agosti, 2015.


Baraza linatoa wito kwa Vikundi vya Sanaa, Wasanii na Wadau wa Sanaa kufanya maandalizi kwa ajili ya kushiriki Maonesho haya.


Baraza linahimiza vikundi, vyama na mashirikisho ya sanaa, wasanii na wadau wa sanaa kutumia fursa hii kuonesha kazi bora za sanaa za Kitanzania.


Aidha, washiriki wote mnatakiwa kujigharamia wenyewe wakati wote wa maonesho.


Kwa maelezo zaidi unaombwa kufika Ofisi za BASATA Idara ya Ukuzaji Sanaa na Masoko au piga simu 0715 825059.


Nakutakia maandalizi mema.


Godfrey L. Mngereza

KATIBU MTENDAJI


Copyright © 2021. All Rights Reserved.