Habari na Matukio

TANGAZO KWA WASANII WOTE

Tarehe: 06/05/2015

YAH: MWALIKO WA KUSHIRIKI MAONESHO YA SANAA NA UTAMADUNI NA SIKU YA AFRIKA TAREHE 20-25 MEI, 2015

Tafadhali rejea kichwa cha habari hapo juu.


Baraza la Sanaa la Taifa limepokea taarifa ya mwaliko tajwa kuwa mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) kwa kushirikiana na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wanaandaa kwa pamoja maonesho ya pili ya Sanaa na Utamaduni na Siku ya Afrika yatakayofanyika kwenye uwanja wa Mwalimu J.K. Nyerere, Dar es Salaam kuanzia tarehe 20 mpaka 25 Mei, 2015.


Lengo la Maonesho haya ni kuwezesha Wasanii na wadau mbalimbali wa tasnia ya Sanaa na Utamaduni kuonesha bidhaa kwa nia ya kupata masoko ya ndani na yale ya nje.


Baraza linahimiza vikundi, Vyama na Mashirikisho ya Sanaa, Wasanii na Wadau wa Sanaa kutumia fursa hii kuonesha kazi bora za sanaa.


Aidha, washiriki watakaohitaji kuwa na banda watapatiwa huduma hiyo kwa gharama ya Tshs 100,000/= + VAT. Banda litakuwa na ukubwa wa mita za mraba tisa (9) meza moja, viti viwili na huduma ya umeme itakuwepo.
Tafadhali thibitisha ushiriki wako kupitia barua pepe: info@tantrade.or.tz, kwa maelezo zaidi unaombwa kufika ofisi za BASATA Idara ya Ukuzaji Sanaa na Masoko au piga simu 0715 825059.

Nakutakia maandalizi mema.


Godfrey L. Mngereza

KATIBU MTENDAJI


Copyright © 2021. All Rights Reserved.