Habari na Matukio

Tarehe: 30/07/2015

WASANII WAELEZWA UMUHIMU WA KUJIWEKEA AKIBA.

Na Mwandishi Wetu


WASANII nchini wametakiwa kujenga utamaduni wa kujiwekea akiba katika mifuko mbalimbali ya jamii kwa kuwa kufanya hivyo kuna kumuhimu mkubwa katika maisha yao baada kuwa wamestaafu kazi zao au wanapokuwa hawana tena uwezo wa kufanya kazi.


Hayo yalisemwa na msanii mkongwe wa maigizo hapa nchini Bakari Mbelemba maarufu kwa jina la Mzee Jangala wakati akizungumza katika Jukwaa la na Sanaa lililofanyika Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) mwanzoni mwa wiki hii jijini Dar es Salaam.


Mzee Jangala alikuwa akijibu hoja iliyotolewa na msanii Christian Kauzeni ambaye alitaka kujua ni kwa nini wasanii wakongwe wengi wanakuwa na maisha magumu licha ya kuwa walifanya kazi nzuri zilizo wajengea umaarufu mkubwa hapa nchini.


Alisema wasanii wengi wakonge hawakuwa na utaratibu wa kuweka akiba, lakini kwa sasa kuna mifuko mingi na mifumo mingi ya kujiwekea akiba hivyo ni muhimu kwa wasanii kujiwekea akiba kwa ajili ya maisha yao ya baadaye.


Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa BASATA, Godfrey Mngereza alisema huu si wakati wa msanii kupata shida baada ya kustaafu au kuzeeka kwa kuwa kuna mifuko mingi ya kuweka akiba na hata ya huduma za afya ambayo kwa mchango kidogo inatoa unafuu mkubwa wahuduma.


"Haipendezi kwa msanii aliyekuwa na jina kubwa au umaarufu katika nchi anapokuwa amepatwa na maradhi kusubili harambee ipite ili apate matibabu, msanii akijiunga na mfumo wa bima ya Afya kwa mfano NHIF analipa fedha kidogo sana na anapata uhakika wa matibabu kwa muda mrefu wa maisha yake," alisema Mngereza.

Copyright © 2021. All Rights Reserved.