Habari na Matukio

Tarehe: 26/09/2019


BASATA NA WASANII WA JAMAFEST 2019 JIJINI DAR ES SALAAM, TANZANIA

Divine Nduwimana, Huyu ni msanii katika fani ya uchoraji kutoka nchini Burundi na nimliki wa kampuni ya Divine-Ndu Art House iliyopo Bujumbura akiwa ni mmoja washiriki wa Jamafest 2019. Kitaaluma Divine ana shahada ya kwanza katika fani ya kilimo.


Katika mahojiano na BASATA anasema tamasha la mwaka huu limefana sana na kulinganisha na lililofanyika nchini Burundi kwani kupitia tamasha hili amejifunza mambo mengi kwanza ukarimu wa watanzania kwa wageni, ustadi na umahiri mkubwa wa kazi za sanaa kutoka kwa wasanii watanzania hivyo katika mpango wake wa baadae kushirikiana na wasanii kutoka Tanzania kufanya nao kazi pamoja lengo ikiwa ni kukuza taaluma ya sanaa kwa nchi za Afrika mashariki.


Copyright © 2021. All Rights Reserved.