Habari na Matukio

Tarehe: 11/10/2019

KUMBUKIZI YA KIFO CHA BABA WA TAIFA, MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE.
Na Mwandishi Wetu

Mwenyekiti wa Bodi,Menejimenti pamoja na Wafanyakazi wote wa Baraza la Sanaa la Taifa-BASATA,inaungana na watanzania wote katika kumbukizi ya kifo cha Baba wa Taifa,Mwalimu Julius Kambarage kilichotokea tarehe 14/10/1999. Sisi kama BASATA,tunatambua na kuenzi mchango wa Baba wa Taifa katika kudumisha na kukuza Utamaduni wetu kupitia Sanaa za ngoma,michezo ya jadi kama vile Bao,uchongaji,Lugha ya Kiswahili nk. Kwani Mwalimu alisema,“TAIFA BILA UTAMADUNI NI TAIFA MFU.”
Na kwa kutambua hilo,Sisi Baraza la Sanaa la Taifa,tutaendelea kudumisha na kuenzi shughuli zote za Sanaa na Utamaduni alizotuachia Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa kusimamia mila na desturi kama vile, maadili ya Kiafarika katika kazi za sanaa hapa nchini.
Kwa pamoja tunasema,tuenzi sanaa na Utamaduni wetu aliotuachia Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho pia.


Copyright © 2021. All Rights Reserved.