Habari na Matukio

Tarehe: 24/10/2019

WAIGIZAJI MAARUFU WA FILAMU YA ODE TO JOY (QIAO XIN NA LIU TAO)WATOA SHUKURANI KWA WATANZANIA.Na Mwandishi Wetu

Wasanii Qiao Xin pamoja na Liu Tao ambao ni waigizaji maarufu katika tamthilia ya Ode to Joy ambayo ilikuwa ikirushwa kupitia king’amuzi cha Star Times nchini Tanzania kwa lugha ya Kiswahili wametoa shukurani zao kwa watanzania hususani washabiki wao kwa kuipokea na kuipenda tamthilia hiku hasa mahudhui yake.
Katika mahojiano na baadhi ya mashabiki wao wa tamthilia ya Ode to Joy jijini Dar Es Salaam, Qiao Xin pamoja na Liu Tao wanasema,tamthilia hiyo inahusu maisha ya wasichana warembo watano ambao wanaisha gorofa ya 20 kwenye jengo la "Happy Ode Community" nchini China.


Licha ya tofauti zao za kitabia ,wanatokea kuwa marafiki wazuri na wenye kuelewana,maisha ambayo wasichana wengi wa kitanzania hususani waishio mijini wameyaishi.


Aidha Qiao Xin na Liu Tao,kwa pamoja wametoa shukurani zao kwa kampuni ya StarTimes nchini Tanzania pamoja na watayarishaji wa tamthilia hii ya Ode to Joy Shandong TV,Media Group pamoja na Daylight Entertainment TV Ltd. kwa kuwezesha kurusha tamthilia hii hapa nchini kwa lugha ya Kiswahili.


Naye Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa(BASATA)Godfrey Mngereza kwa niaba ya Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Harrison Mwakyembe kwanza aliushuruku Ubalozi wa China nchini Tanzania kwa kudumisha ushirikiano wetu tuliojijengea kwa muda mrefu ikiwemo sekta ya Utamaduni.


Bw.Mngereza,katika Mahojiano na Mtangazaji wa chombo cha Habari cha Uchina(China Global Television Network(CGTN) Bi. Shi Yue,anasema,imefika wakati wenzetu pia wa China wakaanza kuonesha filamu zetu zilitengenezwa kwa lugha ya Kiswahili huko kwao kwa lugha ya Kichina ili kusaidia kutangaza Utamaduni wetu.


Kutokana na ukweli kwamba China wamepiga hatua kubwa katika masuala ya teknolojia ya Utangazaji na Mawasiliano, wakaangalia jinsi gani wanavyoweza kuwasaidia wasanii wa Tanzania katika tasnia ya sanaa na Utamaduni ili nao kazi zao ziweze kupata soko la nje ikiwemo nchi ya China.


Wakiwa nchini Tanzania waigizaji hao wa tamthilia ya “Ode to Joy, Qiao na Liu walipata nafasi ya kutembelea maeneo mbali mbali ya kijamii ikiwemo shule ya msingi Mapambano jijini Dar Es Salaam na kutoa zawadi kwa watoto yakiwemo mabegi ya shule,fulana,mipira pamoja na madaftari.
Copyright © 2021. All Rights Reserved.