Habari na Matukio

Tarehe: 25/08/2019

ONGALA FESTIVAL KUENZI MUZIKI WA DANSI NA MUZIKI WA ASILITamasha la Ongala Festival lilliokuwa likifanyika Kwa sikutatu, kuanzia tarehe 23 Agosti na kuhitimishwa tarehe 25 Agosti 2019, katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagomoyo, mkoani Pwani likibeba lengo la kuenzi mziki wa dansi na muziki asili. Tamasha hili liliapa fursa wasanii mbalimbali kushiriki wakiwemo; wasanii kutoka Taasisi hiyo, MamaC kutoka Arusha, Ngoma ya Wakagulu kutoka Morogoro, Shine and dance kutoka Dar-es-salaam na washairi ilihali wadau wa sanaa kutoka Baraza la Sanaa la Taifa walikuwa wageni waalikwa katika Tamasha hilo.


Wasanii kutoka Taasisi ya TaSuBa walifungua Tamasha hilo kisha kufuatia na burudani fupi kutoka kwa MamaC na wengineo huku kikundi cha Shine and dance kikihitimisha kipindi cha burudani. Hata hivyo Sahani ya santuri iliwekwa ili wadau wa Sanaa na washiriki waweze kupata historia fupi ya mkongwe huyo maarufu wa mziki wa Dansi nchini.


Sehemu ya pili ya tamasha hilo ilijumuisha utumbuizaji wa nyimbo za mkongwe huyo wa dansi nchini amabapo washiriki na wadau walipata nafasi ya pekee kufurahia kwa kucheza kutokana na burudani zilizoendelea hadi kufikia ukingoni mwa Tamasha.

Copyright © 2021. All Rights Reserved.