Habari na Matukio

Tarehe: 12/01/2020

DKT. ALLY POSSI ASISITIZA UMOJA MIONGONI MWA WASANIINa Mwandishi Wetu

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Dkt. Ally Possi amesisitiza umoja miongoni mwa wasanii wanaofanya shughuli zao katika eneo la wafanyabiashara wa vinyago lililopo Mwenge jijini Dar Es Salaam ambalo lina mgogoro wa kisheria juu ya umiliki wake.


Mh. Dkt. Possi aliyasema hayo mwishoni mwezi Disemba 2019 alipotembelea na kufanya mkutano na wafanyabiashara hao akiwa katika ziara yake ya kikazi.
“Tunawataka hao wachache wanaoleta huu mgogoro waache wakati na sisi tunaendelea kutatua mgogoro eneo hili. Kikubwa ambacho naomba niendelee kusisitiza ni kuwa wamoja, tukiwa wamoja maendeleo ni ya wote” Alisema Dkt. Possi.


“Jamani, kwa wale ambao hatupo wamoja, je hatuoni aibu..? tuache na tuweni wamoja” alisisitiza Dkt. Possi.


Aidha Dkt. Possi aliahidi kuufanyia kazi na kuumaliza kabisa mogogoro huo kabla mwaka 2020 haujaisha ili wasanii, wadau wa Sanaa na Serikali kwa ujumla wawe huru kuliendeleza eneo hilo ambalo lipo sehemu yenye mvuto wa kibiashara liwe la kisasa kabisa na hatimaye lilete faida za kiuchumi kwa mmoja mmoja na serikali kwa ujumla.

Aidha, Dkt. Possi alitumia nafasi hiyo kulitaka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kukwamua mkwamo wa mradi wa TACIP (Tanzania Arts and Craft Identification Project), jambo ambalo liliwasilishwa katika risala ikiyosomwa na Katibu wa chama hiko Bw.Mintanga Ramadhani risala kama moja ya changamoto wakati Chama cha Wasanii Wachongaji Tanzania (CHAWASAWATA)

Pamoja na hayo Katibu huyo wa CHAWASAWATA alitoa maombi kwa taasisi ya BASATA kutoa tamko juu ya mwongozo wa matumizi ya eneo hilo kwasababu ndiyo waliyokabidhiwa kusimamia eneo hilo kwa tamko la Mheshimiwa Waziri Dkt.Harrison Mwakyembe tangu 20/08/2018.
Copyright © 2021. All Rights Reserved.