Habari na Matukio

Tarehe: 26/09/2019

BASATA NA MSANII KUTOKA RWANDA KATIKA TAMASHA LA JAMAFEST 2019 JIJINI DAR ES SALAAM TANZANIA
Na Mwandishi Wetu

Moja ya kazi nzuri za uchoraji kwenye tamasha la kiutamaduni la jumuiya ya Afrika Mashariki ni kutoka nchini Rwanda ambapo Mchoraji mpFizi Eugene na mmiliki wa MpFiziArt LTD ambaye kuonyesha kazi zake anazochora na vitu anavyotumia kuchora ambavyo ni utamaduni wa kiafrika kutokea nchini Rwanda.


Wanyarwanda wana michoro tofauti kulingana na tamaduni zao kama vile jinsi wanavyocheza,michoro ya vikapu vyao vya kuwekea mazao, Michoro na vyakula mbalimbali wanavyokula kama vile mihogo na samaki vikiwemo pia vyombo vya asili vya kulia chakula.


Michoro hii inachorwa kwa kutumia vitu mbalimbali kama vile mchanga, unga unaotokana na miti, magamba ya miti na magamba(shells) ya Konokono.


Msanii mpFizi Eugene anasema,Changamoto kubwa wanayokutana nayo hususani wachoraji kutoka Rwanda ni ukosefu wa wateja ambao ni wachache sana wanaokuja kutembelea banda lao wakati katika tamasha hili wamekuja na vitu vingi vizuri kutoka nchini kwao na itawawia vigumu kurudi navyo.


Ombi lao kwa wadau wa Sanaa kutoka nchini Tanzania nan chi washiriki wa Jamafest 2019 ni kuwapa ushirikiano kwa hizi siku zilizobakii waje kujionea kazi mbali mbali kutoka kwao na kununua kazi za Sanaa kutoka Rwanda kwa ajili ya mauzo ambapo wanaweza kuingia makubaliano nao baada ya kuziuza wakawatumia hela kulingana na makubaliano kati ya wasanii kutoka Rwanda na Watanzania.


Copyright © 2021. All Rights Reserved.