Habari na Matukio

TANGAZO KWA WASANII NA WADAU WOTE WA SANAA

Tarehe: 05/08/2015

YAH: TAMASHA LA NANE LA KIMATAIFA LA KUIMBA NYIMBO ZA DINI PAMOJA NA ZA SUFI MUSIC, CAIRO - MISRI

Baraza la Sanaa la Taifa limepokea barua toka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo juu ya Tamasha tajwa linalotarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 20/09/2015 mpaka 27/09/2015.


Baraza linahimiza vikundi, vyama, mashirikisho ya sanaa, wasanii na wadau wa sanaa kutumia fursa hii kuonyesha kazi bora za sanaa.


Aidha, washiriki wote wanatakiwa kujigharamia wenyewe usafiri wa kwenda na kurudi pamoja na mizigo yao. Nchi wenyeji itagharamia usafiri wa ndani, chakula, malazi, na matangazo katika vyombo vya Habari.


Kwa maelezo zaidi unaombwa kufika ofisi za BASATA, Idara ya Ukuzaji Sanaa na Masoko au piga simu namba 0789 094477.


Nakutakia maandalizi mema.


Godfrey L. Mngereza

KATIBU MTENDAJI


Copyright © 2021. All Rights Reserved.