Habari na Matukio

Tarehe: 20/10/2019

BASATA YAWAPONGEZA Diamond, Rayvanny na Nandy kushinda Tuzo Marekani

Na Mwandishi Wetu

Wasanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, Rayvanny na Nandy mwishoni wa wiki hii(Jumapili) wameshinda tuzo ya African Entertainment Awards USA (AEAUSA) nchini Marekani. Nasibu Abdul Juma(Diamond Platnumz) ameshinda tuzo ya African Entertainment Awards USA (AEAUSA) kwenye kipengele cha ‘Best Collaboration Award’ kupitia wimbo wake wa Baila.
Huku Raymond Shaban Mwakyusa( Rayvanny) msanii mwenye sifa kubwa katika kuandika mashairi ya Muziki na Uimbaji akiwa amejishindia tuzo ya (Best Male in East,South and North Africa).


Ambapo kwa upande wa msanii wa kike,muimbaji na mtunzi wa nyimbo, Faustina Charles Mfinanga (Nandy) kutoka pia Tanzania akiibuka mshindi katika shindano la African Entertainment Awards USA (AEAUSA) kwenye vipengele cha Best Female in East, South and North Africa.
BASATA likiwa ni msimamizi na mratibu wa kazi za sanaa hapa nchini, linatoa pongezi za dhati kwa Wasanii hawa Nandy, Rayvanny pamoja na Diamond Platnumz kwa ushindi wa Tuzo ya African Entertainment Awards USA 2019(AEAUSA)na kuliletea Taifa heshima. Hii ni ishara kwamba wasanii wetu wanakubalika ndani na nje ya Tanzania,hivyo basi Ushindi huu uwe ni fursa ya kupanua wigo wa kazi zao kuingia katika soko la kimataifa Zaidi. Imetolewa na: Kitengo cha Habari na Mawasiliano-BASATA


Copyright © 2021. All Rights Reserved.