Habari na Matukio

Tarehe: 28/09/2019

MAANDALIZI YA SHINDANO LA MISS UTALII 2019/2020LAZIDI KUPAMBA MOTO
Na Mwandishi WetuUtalii Tanzania mwaka 2019-2020 Georgina Saulo amesema hadi sasa kazi kubwa iliyofanya kwa mujibu wa kanuni na sheria zilizowekwa na bodi ya Miss Utalii Tanzania,kwa kuzingatia Ushauri wa Basata hiyo ni pamoja na: Georgina Saulo-Mkurugenzi wa Mashindano na Matukio (Miss Utalii Tanzania 2019/2020 • Muundo mpya wa uongozi na mashindano kama ulivyopitishwa na Basata • Kwamba asilimia 95 ya Maandalizi kwa ajili ya semina kwa waandishi wa Habari na waratibu wa kanda wa shindano la Miss Utalii Tanzania yamekamilika.
semina hii itafanyika kati kati ya mwezi huu wa 10,2019 katika hoteli ya Jaromax palace jijini Dar Es Salaam huku Baraza la Sanaa la Taifa ikiwa ni mgeni mwalikwa,lengu kuu likiwa ni kuwafanya washiriki kuelewa kanuni,taratibu za shindano hili,lakini pia wajue nini maanda ya Sanaa za Urembo.
Bi.Georgina Saulo,anasisitiza kwamba, Sharti mojawapo la kuwa Mratibu katika shindano hili ni lazima uwe umesajiliwa na Baraza la Sanaa Tanzania-BASATA na kwa upande wa washiriki(warembo)moja ya sharti la kushiriki ni lazima awe ni raia wa Tanzania na mwenye taswira nzuri kwa jamii ya Kitanzania.
Aidha mchakato wa kuwapata warembo katika ngazi za kanda unategemea kuanza rasmi mwezi Nov,2019 hadi March 2020 Hivyo Mkurugenzi wa Mashindano na Matukio ya Miss Utalii Tanzania mwaka 2019-2020 Georgina Saulo amewataka wale wote wanaotaka kushiriki shindano la Miss Utalii Tanzania yaani Waratibu pamoja na warembo wenye nia ya kutaka kushiriki wajitokeze kwa wingi kuchukua fomu kwani Miss Utalii Tanzania 2019/20 imekuja kivingine.


Washiriki zaidi ya 100, wenye mataji ya kitakaifa kutoka zaidi ya nchi 100 duniani watashiriki shindano la kimataifa la Miss Utalii Tanzania 2019/2020 litakalo fanyika nchini Tanzania Juni 2020. Miss Utalii Tanzania ni alama ya Urithi wa Taifa,Utalii ni maisha,Utamaduni ni Uhai wa Taifa(Miss Tourism Tanzania,the symbol of national Heritage ,Tourism is life, Culture is Living)
Copyright © 2021. All Rights Reserved.