Parliament Logo

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Baraza la Sanaa la Taifa

BASATA VIBES

12 Sep, 2025
BASATA VIBES

Basata Vibes
Basata Vibes ni jukwaa la ubunifu, burudani na maarifa linaloandaliwa na
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) likiwa na lengo la kuimarisha na kuendeleza
sekta ya sanaa na ubunifu nchini Tanzania. Hii ni sehemu maalum
inayokutanisha wasanii, wabunifu, vijana na wadau wa sanaa ili kushirikiana,
kujifunza na kuibua fursa za kijamii na kiuchumi kupitia sanaa.
Malengo ya Basata Vibes
 Kuwezesha vijana na wasanii kupata jukwaa la kuonesha vipaji vyao
kwa hadhira pana.
 Kuchochea ubunifu na maarifa kupitia midahalo, warsha, na mijadala
ya kisekta.
 Kujenga mtandao wa ushirikiano kati ya wasanii, taasisi, na wadau
wa sekta.
 Kukuza fursa za ajira na biashara zinazotokana na tasnia ya sanaa na
ubunifu.
 Kuhamasisha jamii kutambua mchango wa sanaa katika maendeleo ya
kijamii na kiuchumi.
Vipengele vya Basata Vibes
 Maonesho ya sanaa na ubunifu – nafasi ya kuonesha kazi za sanaa za
uchoraji, muziki, maigizo, filamu, mitindo, ngoma za asili, na bidhaa
bunifu.
 Burudani na matamasha – jukwaa la muziki na maigizo ya moja kwa
moja yanayowakutanisha wasanii wakongwe na chipukizi.
 Mijadala na midahalo – majukwaa ya kujadili changamoto na fursa
katika sekta ya sanaa na ubunifu.

 Mafunzo na warsha – kuwajengea wasanii ujuzi katika masuala ya
kibiashara, masoko, haki miliki, na matumizi ya TEHAMA.
 Mitandao na ubia – kusaidia wasanii kupata ushirikiano na wadau wa
ndani na nje ya nchi.
Umuhimu wa Basata Vibes
Basata Vibes ni zaidi ya burudani—ni jukwaa la kuunganisha jamii kupitia sanaa,
kukuza mazungumzo yenye tija, na kutoa nafasi kwa vijana kutumia ubunifu wao
kutatua changamoto za kijamii. Kupitia jukwaa hili, BASATA inaendeleza dhamira
yake ya kuhakikisha sanaa inathaminiwa, inalinda mila na utamaduni wa
Kitanzania, na kuchangia kikamilifu katika maendeleo endelevu ya Taifa.
Maono ya Muda Mrefu
BASATA inalenga kulikuza Basata Vibes kuwa moja ya matukio makubwa na
yenye ushawishi barani Afrika katika sekta ya sanaa na ubunifu. Kwa muda,
jukwaa hili linatarajiwa:
 Kuwa brand ya kitaifa na kikanda inayotambulika kimataifa.
 Kupanua ushiriki wake kwa kujumuisha wasanii na wabunifu kutoka Afrika
Mashariki na kwingineko.
 Kuwezesha ubunifu wa Kitanzania kufika katika soko la kimataifa.
 Kuwa kituo cha elimu na ubunifu endelevu, kinachochangia kwa dhati
katika mapinduzi ya uchumi wa ubunifu nchini.
Matarajio ya Basata Vibes
 Kila toleo jipya la Basata Vibes kuwa na kaulimbiu mahususi inayojikita
katika changamoto au fursa za kisasa.
 Kufikia vijana wengi zaidi kwa kutumia teknolojia za kidijitali na
majukwaa ya mitandaoni.

 Kuwa daraja la ajira na biashara kwa wasanii kupitia maonesho,
mafunzo na ubia wa kimkakati.
 Kuendeleza ushirikiano wa kikanda na kimataifa kwa ajili ya kukuza
thamani ya sanaa ya Tanzania.

Settings