
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) lililoundwa kwa lengo kuu la kufufua na kuendeleza kazi za
sanaa na kufanya tafiti mbalimbali za masuala ya Sanaa ambazo sanaa hizo zimeweza
kugawanywa katika sehemu kuu tatu ikiwemo Sanaa za Ufundi, Muziki na Sanaa za Maonesho.
Baraza la Sanaa la Taifa limeweza kusaidia kusajili wadau mbalimbali wanao jishughulisha na
kazi za sanaa ili kuweza kupata vibali ambavyo vitawasaidia kufanya na kuonesha kazi zao za
Sanaa katika jamii.
Sanaa za Ufundi
Sanaa za ufundi ni sanaa ambazo huusisha utengenezaji wa vitu mbalimbali kwa kutumia
mikono, sanaa hizi zinawafanya watu kuweza kujishughulisha kutengeneza vitu ikiwemo nguo,
mikoba, samani, vinyago, nakadhalika.
Sanaa za ufundi zipo za aina mbalimbali ambazo zinatofautiana kulingana na jinsi
zinavyoonekana katika macho ya watu, zilivyotengenezwa au kusanifiwa katika muonekano
tofauti tofauti na kuweza kuzitofautisha kwa zinavyoonekana sanaa hizo ni kama vile; Urembo,
utanashati, ulimbwende, ubunifu wa mavazi, uwana mitindo, uchoraji, upakaji rangi, usanifu
maumbo, ususi na unyoaji, upambaji wa keki, upambaji wa matukio, ufinyanzi, upigaji picha
mnato, uchongaji, udarizi, ufumaji, ushonaji nakadhalika.
Mikakati ya Sanaa za Ufundi ni kuhakikisha inatoa elimu kwa wadau wa sanaa ikiwemo elimu
ya kujisajili ili kuwawezesha wadau hao kutangaza sanaa zao sehemu mbalimbali na kuweza
kupata fursa za kibiashara pamoja na vibali. Vilevile, kutafuta masoko ya kuuza bidhaa zao,
masoko hayo ikiwemo kutoa elimu juu ya kutumia mitandao ya kijamii kujitangaza na kuonesha
bidhaa zao kupitia mitandao hiyo, pia kuandaa maonesho kwa wafanya sanaa za vitendo kama
ususi, ulimbwende, ufinyazi nk.
Katika Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Sanaa za Ufundi hushirikiana na Shirikisho la
Tanzania Federation of Crafts and Arts (TAFCA) shirikisho hilo husaidia kazi za Serikali
kutekeleza shughuli fulani ambapo shirikisho huundwa na vyama vidogo vidogo ilikuweza
kushiriki katika mambo mbalimbali ya kimaendeleo ikiwemo na Sanaa.
Kwa ujumla Sanaa za Ufundi kwa kushirikiana na shirikisho hilo limesaidia kuitangaza Sanaa
hiyo mpaka nje ya Taifa kutokana na uwepo wa wadau mbalimbali wa Sanaa wakiwemo
wachoraji, wafumaji, wachongaji vinyago hii ni kutokana na kuandaliwa na kualikwa katika
matamasha mbalimbali ya nje na kuweza kutambulika kwa Sanaa za Ufundi kutokana na bidhaa
zao.
Mambo Muhimu ya Kujumuishwa kwenye Tovuti kuhusu Sanaa za Ufundi
BASATA
1. Utangulizi
Historia fupi ya BASATA na dhamira yake kuu katika kuendeleza sekta ya sanaa
nchini.
Maelezo ya jumla ya aina kuu za sanaa zinazoratibiwa (Muziki, Maonesho,
Ufundi).
2. Maelezo ya Sanaa za Ufundi
Ufafanuzi wa Sanaa za Ufundi ni nini.
Mifano ya kazi zinazohusiana (uchongaji, ushonaji, ufinyanzi, urembo, n.k.).
Umuhimu wake kiuchumi, kijamii na kiutamaduni.
3. Malengo na Majukumu ya BASATA katika Sanaa za Ufundi
Kusaidia wasanii kusajiliwa rasmi na kupata vibali.
Kuwezesha uanzishaji wa vikundi vya sanaa.
Kutoa elimu ya kibiashara na masoko.
Kuwezesha ushiriki wa wasanii katika maonesho ya ndani na nje ya nchi.
4. Mikakati Mikuu ya BASATA katika Kukuza Sanaa za Ufundi
Elimu ya kujisajili na kupata leseni.
Mafunzo ya ujasiriamali na matumizi ya mitandao ya kijamii.
Kuandaa maonesho ya sanaa za mikono.
Kuunganisha wasanii na masoko ya ndani na nje ya nchi.
5. Ushirikiano wa BASATA na TAFCA
Jukumu la TAFCA (Tanzania Federation of Crafts and Arts).
Namna vyama vya wasanii wanavyoshirikiana kupitia TAFCA.
Mafanikio ya pamoja katika kukuza sanaa za ufundi.
6. Mafanikio Makubwa
Ushiriki wa wasanii wa Tanzania katika matamasha ya kimataifa.
Uongezekaji wa fursa za biashara kwa wasanii.
Utambulisho wa kazi za mikono kutoka Tanzania kimataifa.
7. Fursa kwa Wasanii wa Ufundi
Namna ya kujiunga/kusajiliwa BASATA.
Kozi au mafunzo yanayotolewa.
Ratiba za maonesho au matamasha.
Fursa za masoko ya kimataifa na mitandao ya kijamii.