UJUMBE WA KATIBU MTENDAJI
Dkt. Kedmon Mapana
Kwa niaba ya Menejimenti na Watumishi wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA),
napenda kukukaribisha kwenye tovuti yetu rasmi. Tovuti hii imebuniwa kuwa
jukwaa mahsusi la mawasiliano kati ya BASATA na wadau mbalimbali wa sanaa
ikiwemo wasanii, wanajamii, taasisi za Serikali, sekta binafsi, na wadau wa
maendeleo.
Kupitia ukurasa huu utapata taarifa sahihi, za kina, na za kuaminika kuhusu
huduma tunazotoa, sera na miongozo ya sekta ya sanaa, matukio muhimu,
pamoja na mikakati ya kukuza na kuendeleza sanaa nchini.
BASATA, kama taasisi ya Serikali yenye dhamana ya Kukuza na Kuendeleza
Sanaa Tanzania, limeendelea kuwa mshirika wa karibu katika kukuza vipaji,
kuhamasisha ubunifu, na kuhakikisha tasnia ya sanaa inachangia kikamilifu
katika maendeleo ya kiuchumi, kijamii, na kiutamaduni ya Taifa letu.
Tukiwa na wataalamu wenye weledi na uzoefu mkubwa, tunahakikisha tunatoa
mwongozo na huduma bora zinazojenga mazingira wezeshi ya ustawi wa sekta
ya sanaa. Tunakuaribisha kutumia tovuti hii kama nyenzo ya kupata taarifa,
kushirikiana nasi, kutoa maoni, na kujifunza zaidi kuhusu nafasi ya sanaa katika
maendeleo ya Taifa.
BASATA itaendelea kujidhatiti kuhakikisha kuwa sekta ya sanaa inakuwa chachu
ya ajira, mshikamano wa kijamii, urithishaji wa tamaduni, na ukuzaji wa uchumi
wa ubunifu.
Karibu sana kwenye tovuti ya BASATA – chombo chako cha kuaminika katika
ustawi wa sanaa Tanzania.