Parliament Logo

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Baraza la Sanaa la Taifa

Katibu mkuu TAMISEMI ahimiza uharaka wa kuunganish...

22 Jan, 2025
Katibu mkuu TAMISEMI ahimiza uharaka wa kuunganisha mfumo wa AMIS na TAUSI

Katibu mkuu TAMISEMI ahimiza uharaka wa kuunganisha mfumo wa AMIS na TAUSI

Na Isack N. Bilali

Katibu Mkuu TAMISEMI ndugu Adolf H. Ndunguru amepongeza watumishi na uongozi wa BASATA na TAMISEMI kwa ushirikiano waliouanza katika kuhakikisha mifumo ya AMIS na TAUSI inaunganishwa na kusomana jambo ambalo litasaidia kurahisisha ufanisi wa utoaji huduma za kiuchumi kwa wananchi na Serikali.

Ameyasema hayo tarehe 05 Disemba, 2024 wakati akiongea na watumishi na uongozi wa BASATA na TAMISEMI ambao wamekutana katika ukumbi wa Forest Sun set Mjini Morogoro ambapo amewataka kuongeza kasi ya ufanyaji kazi ili mifumo hiyo ianze kufanya kazi katika mwaka wa fedha 2024/2025 kama ilivyopangwa.

Ameendelea kusema kuwa suala la mifumo ya serikali kusomana siyo la hiyari bali ni maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan wataalamu wamehimizwa kumaliza vipengele vilivyosalia ikiwemo suala la kisheria ili mifumo hii ikiungana yasainiwe makubaliano thabiti yatakayokuwa na uhalali wa kisheria hivyo kutoa faida kwa vizazi vya baadae nchini.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Gerson Msigwa ametoa shukrani kwa Wizara ya TAMISEMI na wataalamu wake wakiongozwa na Katibu Mkuu wao kwa namna walivyolibeba jambo hilo kimkakati zaidi.

Ametoa wito kwa Baraza la Sanaa la Taifa kutumia ubunifu wa hali ya juu kuhakikisha wanatoa elimu ya kutosha kwa wadau wake ili waweze kuelewa faida ya  matumizi ya mfumo.

Kikao hicho kimewakutanisha viongozi Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, BASATA na TAMISEMI ikiwa ni kikao kazi cha kupitia na kuona maendeleo ya uunganishaji wa mfumo wa TAUSI na AMIS katika ukumbi wa Forest Sun set Mjini Morogoro.

Settings