

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ni Shirika la umma lililoundwa kwa Sheria ya Bunge Na. 23 ya Mwaka 1984 kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sheria Na. 5 ya Mwaka 2019. Historia inaonyesha kuwa, Sheria ya kuunda upya Baraza hili ilifanywa kwa kuunganishwa Sheria ya Baraza la Sanaa la Taifa ya Mwaka 1974 na Baraza la Muziki la Taifa (BAMUTA) ya Mwaka 1974. Baraza liliundwa ili lisimamie maendeleo ya sanaa nchini
Dira
Kuwa chombo chenye uwezo wa hali ya juu wa kutoa huduma bora kitaifa katika maendeleo ya sanaa
Lengo kuu
Kufufua, kukuza na kuongeza maendeleo ya utengenezaji wa kazi bora za Sanaa.
Maadili
Maadili ya msingi ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ni kuhimiza na kukukuza utamaduni halisi wa sanaa ya Kitanzania,
kudumisha ubobezi na ubora wa hali ya juu na kuchochea ubunifu na uvumbuzi katika sanaa
- Limepania kuhimiza na kukuza utamaduni halisi wa sanaa ya Kitanzania
- Limepania kudumisha ubobezi na ubora wa hali ya juu
- Limepania kuhimiza ubunifu na uvumbuzi katika sanaa