Parliament Logo

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Baraza la Sanaa la Taifa

TAFCA WAKUTANA KATIKA KIKAO CHA MWAKA KUJADILI MIP...

22 Jan, 2025
TAFCA WAKUTANA KATIKA KIKAO CHA MWAKA KUJADILI MIPANGO MIKAKATI

Shirikisho la Sanaa za Ufundi Tanzania (TAFCA) limefanya kikao chake cha mwaka kilichoongozwa na Katibu Mtendaji wa BASATA, Dkt. Kedmon Mapana, kwa madhumuni ya kujadili na kuandaa mipango mkakati ya mwaka kwa ajili ya kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na weledi. Kikao hicho muhimu kilihudhuriwa pia na Rais wa Shirikisho hilo, Bw. Adrian Nyangamale, ambaye aliongoza mjadala wa kuweka vipaumbele vya maendeleo na malengo madhubuti ya kuimarisha sekta ya sanaa za ufundi nchini. Wajumbe walijadili kwa kina hatua za kimkakati zitakazochangia ukuaji endelevu wa shirikisho na sekta ya sanaa kwa ujumla.

Settings