1.1 MAJUKUMU YA BARAZA LA SANAA LA TAIFA
Kulingana na kifungu cha 4(1) cha Sheria ya Uanzishwaji wa Baraza la Sanaa la Taifa namba 23 ya mwaka 1984 na marekebisho yake ya mwaka 2019. Baraza la Sanaa la Taifa lina majukumu yafuatayo:
- Kufufua na kuhimiza maendeleo ya kazi za Sanaa;
- Kufanya tafiti za masuala mbalimbali ya Sanaa;
- Kusajili wasanii na miundombinu ya Sanaa nchini;
- Kutoa ushauri na misaada ya kitaalamu kwa Asasi au watu wanaojihusisha na shughuli za Sanaa;
- Kuratibu shughuli za Sanaa zinazofanywa na watu au Taasisi mbalimbali;
- Kutoa na kuimarisha mipango ya mafunzo kwa wadau wa Sanaa;
- Kuishauri Serikali juu ya mambo yanayohusu maendeleo na uzalishaji wa kazi za Sanaa;
- Kuhamamsisha maendeleo ya Sanaa kwa njia ya maonesho, mashindano, matamasha, warsha na semina;
- Kusajili wasanii na wadau wanaojihusisha na kazi za Sanaa;
- Kuandaa miongozo ya kusimamia ubora wa kazi za Sanaa;
- Kutunza kanzidata za wasanii na wadau wanaojishughulisha na kazi za Sanaa
- Kuendesha na kusaidia taasisi au watu wanaojishughulisha na kutengeneza, kuingiza, kusafirisha au kuuza nje ya nchi kazi za Sanaa;
- Kuhimiza uzingatiaji wa maadili na tamaduni za Kitanzania katika kazi za Sanaa miongoni mwa wasanii na wadau wa Sanaa;
- Kuhimiza uanzishwaji wa vyama au mashirikisho ya Sanaa kwa lengo la kuongeza idadi ya vikundi vinavyojishughulisha na kazi za Sanaa;
- Kuwezesha wasanii wazawa au vikundi vya Sanaa kupata mafunzo au kuongeza ujuzi ndani au nje ya nchi;
- Kuchangisha na kusimamia fedha zitakazopatikana kutoka vyanzo mbalimbali ili kuliwezesha Baraza la Sanaa la Taifa na wasanii kutekeleza majukumu yao; na
- Kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya watu, vikundi, taasisi, vyama, au wamiliki wa miundombinu wanaojishughulisha na kazi za Sanaa kwa kukiuka Sheria ya Baraza la Sanaa la Taifa.