Parliament Logo

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Baraza la Sanaa la Taifa

MUSIC SECTION-BASATA

12 Sep, 2025
MUSIC SECTION-BASATA

SEHEMU YA MUZIKI – BASATA


Muziki ni Sanaa ya kupanga sauti  na kimya kwa namna
yenye mpangilio na muundo maalumu ili kuwasilisha hisia
au mawazo.(Merriam,1964). Mpangilio wa Sauti
hizi hujumuisha melodia (mdundo wa sauti),harmonia (mchanganyiko wa sauti)
na ritmo(mpangilio wa midundo).


Tansnia ya muziki nchini Tanzania umepitia katika vipindivitatu ambavyo ni ;
 Kabla ya ukoloni
 Kipindi cha ukoloni
 Baada ya ukoloni (Baada ya uhuru).


KABLA YA UKOLONI.


Muziki nchini Tanzania kabla ya ukoloni ulikuwa sehemu ya maisha ya
kila siku katika jamii za kiafrika .
Muziki katika kipindi  hichi ulikuwa na majukumu kwenye  sherehe,ibada na kazi
za jamii ambapo ulitumika katika;
• Kuelimisha jamii
• Kuhamasisha jamii katika kilimo,uvuvi
• Kutunza historia ya  koo
• Kusifia mashujaa
Muziki huo ulitumia vyombo vya
 asili kama ngoma,zeze,filimbi,marimba na kayamba.
Pia katika  kipindi hichi
 hakukuwa na mfumo rasmi wa kusimamia muziki,muziki ulikuwa ukidhibitiwa na 
mila na wazee wa jadi.
Vilevile muziki huu ulipitishwa vizazi hadi vizazi  kupitia njia ya  mdomo(oral
tradition).


KIPINDI CHA UKOLONI (karne ya 19).


Tanzania  (tanganyika)ilipitia utawala wa kijerumani(1880s-1919)
na kisha kiingereza (19191-1961).kipindihichi
muziki ulipitia mabadiliko kutokana na mwingilianowa tamaduni .
 Muziki wa jadi kuchanganyika na muziki
wa kigeni.wamisionari walileta nyimbo za dini (madras,kwayaza kikristo)
 Muziki ulianza kutumika kibiashara zaidi, mwazonikarne  ya 20 muziki
wa dansi  ulianza kuenea kupitiandogondogo .
Miji kama Dar  es Salaam, Tanga,zanzibar ikawa vivutiovya muziki
wa dansi ,taarabu na muziki wa pwani .

 Muziki kuanza kutumika katika mashindano na burudani. 
Waingereza walihamasisha muziki kwenye maonesho ya jamii (community  fairs
)lakini mara nyingi walidhibitimaudhui.


KIPINDI BAADA YA UKOLONI(Baada ya uhuru).


Baada ya Tanganyika  kupata uhuru mwaka 1961 na zanzibar mwaka 1963
,muziki ulitumwa kama chombo cha kujenga utaifa na mshikamano .
Serikali  ya Mwl.julius .Nyerere  ilitumia muziki kama
sehemu ya siasa ya ujamaa na kujitegemea(socialism and self reliance).
Vikundi vya Sanaa vya taifa  na
vya mikoa vilianzishwa ili kuhamasisha uzalendo .
Bendi kubwa kama NUTA Jazz band, JUWATA JAWA ,MLIMANI
PARK zilipata umaarufu  .
Muziki wa dansi ,kwaya ya kisiasa ,taarabu ziliungwa mkono na serikali.
Kiubuka kwa muziki wa kidijitali na midundo mipya(reggae ,disco ,pop).
Pia vijana walianza midundo  ya hip hop na brakedance.
Changamoto  zilizojiitokeza katika muziki kipindibaada ya ukoloni.
• Maudhui  yasiyo na maadili ya kuendana na mila na tamaduni za kitanzania
• Ukosefu wa uratibu  wa sekta ya muziki.


KUANZISHWA KWA BASATA .


Kupitia Sheria  Na 23 ya mwaka 1984 ,serialised iliundabaraza la Sanaa la taifa (
BASATA) chini ya wizard ya michezo ,Sanaa na utamaduni .
BASATA ikapewa jukumu la kusimamia ,kukuza na kulinda Sanaa zote pamoja
na muziki .
Kwa nini Tanzania  iliamua kuanzisha BASATA.
• Kulinda maadili ya Taifa ,baadhi
 ilianza kukosamaudhui ya kiTanzania
• Kudhibiti na kukuza ubora wa kazi za muziki.
• Kurahisisha usajili na uratibu (kuwepo chombokimoja
cha serikali  cha kusimamia  vikundi ,matamasha  na shughuli za
muziki).
• Kukuza utambulisho wa kitanzania   ,kupitiamuziki wa asili ambao ni
writhing wa utamaduniwa taifa .

1. Historia ya Sehemu ya Muziki


Sehemu ya Muziki ilianzia kutoka taasisi ya BAMUTA (Baraza la Muziki la Taifa)
iliyoanzishwa mwaka 1974 kwa lengo la kusimamia, kudhibiti, na kukuza muziki

wa Tanzania. BAMUTA ilikuwa na jukumu la kuhakikisha miziki ya nje
inadhibitiwa huku ikikuza muziki wa asili. Mnamo mwaka 1984, BAMUTA
iliunganishwa rasmi ndani ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kupitia Sheria
Na. 23 ya mwaka 1984. Tangu hapo, shughuli zote za usimamizi wa muziki
zilihamishiwa kwenye Sehemu ya Muziki ndani ya BASATA.


2. Wajibu wa Sehemu ya Muziki
Sehemu hii inaratibu shughuli zote za muziki nchini ikiwemo usajili wa wasanii,
utoaji wa vibali, udhibiti wa maudhui, uhamasishaji wa maadili, na uratibu wa
matukio ya muziki kwa lengo la kukuza sekta hiyo.


3. Majukumu na Malengo
Majukumu ni pamoja na:
 Kuendeleza muziki wa asili na wa kisasa nchini.
 Kusajili wasanii wa muziki na vikundi vyao ili watambulike kisheria.
 Kutoa vibali kwa ajili ya maonesho ya muziki na shughuli zinazohusiana.
 Kusimamia maudhui ya kazi za muziki ili kuhakikisha yanazingatia maadili ya
taifa.
 Kutoa elimu kwa wasanii kuhusu haki, wajibu na fursa zilizopo katika tasnia
ya muziki.


4. Usajili wa Wasanii
BASATA husajili wasanii binafsi na vikundi vya muziki kupitia taratibu rasmi.
Usajili una malengo makuu yafuatayo;
.kutambua rasmi shughuli za wasanii na vikundi vyao.
.kuwezesha wasanii kupata haki zao kisheria.
.kuratibu na kudhibiti ubora wa kazi za muziki.


AINA ZA USAJILI.


BASATA husajili;


Wasanii binafsi(solo artists).
Vikundi vya muziki(music bands/groups)
Makampuni ya muziki
Majukwaa ya burudani na studio za muziki.


VIGEZO VYA USAJILI.

Msanii awe na nakala ya kitambulisho halali (NIDA,leseni au pasipoti).
Picha ya pasipoti .
Msanii awasilishe maelezo ya kazi anazofanya(aina ya muziki,uzoefu).


GHARAMA ZA USAJILI.


Gharama hizi hulipwa pale msanii anaposajisajili kwa mara ya kwanza na
hulipwa kwa mwaka.
Msanii binafsi -Tzs 10,000/=
Vikundi vya muziki -Tzs-20,000/=
Makampuni -Tzs 100,000/= -300,000/.


FURSA ANAZOPATA MSANII /WASANII ANAPOJISAJILI.


Kutambulika kisheria.
Kupata fursa za kushiriki katika tuzo mbalimbali za muziki kama Tanzania
Music Awards (TMA).
Kupata barua za utambulisho kwenye matukio ya kitaifa na kimataifa.

 

6. Masuluhisho Yanayofanywa na BASATA


 Kufanya mapitio ya sheria na kanuni ili kuwa na uwiano sahihi.
 Mapitio na uhuishaji wa sera ya utamaduni ya 1997.
 Kutoa elimu ya usajili kupitia kampeni za kitaifa na vyombo vya habari.

 

 Kukagua kazi za muziki kabla ya kuruhusiwa kusambazwa.
 Kutoa adhabu/faini kwa wanaokiuka maadili ya muziki.
 Kutoa semina na mafunzo ya biashara ya muziki kwa wasanii.
 Kuanzisha programu za kuifikia jamii ya wasanii wa vijijini.


7. Matukio Muhimu ya Muziki


Sehemu ya Muziki inashiriki katika kuratibu na kushiriki matukio mbalimbali ya
kitaifa yanayochochea maendeleo ya muziki. Mifano ya matukio hayo ni:TMA
zilianzishwa kwa dhumuni la kutambua mchango wa wasanii katika tasnia ya
muziki.
Kuinua kiwango cha ubora wa kazi.
Kukutanisha wasanii na wadau wa kimataifa wa Sanaa na burudani
 Tanzania Music Awards (TMA): https://www.tmaa.co.tz

8. Hitimisho


Sehemu ya Muziki ni chombo muhimu katika kukuza na kuendeleza kazi za
muziki kwa kuzingatia sheria, maadili na ubunifu. BASATA inawahimiza wasanii
kushirikiana kwa karibu na taasisi hii ili kuhakikisha maendeleo chanya ya tasnia
ya muziki kwa manufaa ya taifa zima.

Settings