Naibu katibu Mkuu aipongeza BASATA
Naibu Katibu mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Methusela Stephen Ntonda ameipongeza Menejimenti ya baraza la sanaa la TAifa na kuwataka waongeze ubunifu katika utekelezzaji wa shughuli za kuenedleza sekta ya sanaa nchiniili kuongeza msukomo kwa wasanii katika kujiongezea kipato.
Ameyasema hayo tarehe 10 Agosti, 2024 wakati anaongea na timu ya wakuu wa idara na vitengo baada ya kutembelea ofisini hapo kwa minajili ya kujitambulisha na kutambua majukumu ya kuendeleza zsekta ya sanaa yaliyowasilishwa na Katibu Mtendaji Dkt. Kedmon Mapana katika taarifa ya utekelezaji.
Naibu Katibu mkuu ametanabaisha misingi ya utendaji wa kazi iambatane na ubunifu wa majukumu bila kuathiri taratibu huku lengo likiwa kukamilisha kwa mafanikio mikakati yote iliyopangwa katika taasisi kwa kipindi husika cha utekelezaji.
“Taasisi lazima iwe na mipango thabiti itakayokupa dira thabiti inayokuonesha umefika wapi na kama kuna mkwamo upo sehemu gani ili iwe arahisi kupata suluhisho, kwahiyo watumishi waongeze ubunifu ili kuweza kupiga hatua mbele zaidi” amesema Bw. Ntonda.
Alipogusiwa suala la changamoto ya mmomonyoko wa maadili katika sekta ya sanaa, Bw. Ntonda ameipongeza BASATA kwa kuwa na mwongozo wa uzingatiaji wa maadili katika shughuli za sanaa ambao umesambazwa kwa wadau wake, ila amesisitiza kuwa jambo hili ni mtambuka isiishie hapa washirikishwe na taasisi zingine ili na wao waweze kuwafikia jamii mzima.
“Suala la maadili linaendana na tabia ya mtu, watu na jamii kwa ujumla hivyo yapasa kuongeza nguvu katika ushirikishwaji ili kuwafikia taasisi zingine zisaidie kupaza sauti kwa jamii yote” ameongeza Ntonda.
Naibu Katibu Mkuu amefanya ziara hiyo ikiwa ni sehemu ya kutembelea na kujitambulisha kwa watumishi wa taasisi zote zilizo chini ya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo mara baada ya kuteuliwa kushika nyadhifa hiyo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na kuapishwa Agosti mwaka huu.