
viongozi kutoka Tume ya Utumishi wa Umma wamefanya ziara ya kikazi katika Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa lengo la kukagua na kuangalia utekelezaji wa taratibu za Utumishi wa Umma ndani ya taasisi hiyo mbapo wamefanya ziara hiyo Oktoba 20,2025
Ujumbe wa Tume hiyo umeongozwa na Kamishna wa Tume, Bw. Hassan Kitenge, akiwa ameambatana na Mkurugenzi wa Huduma za Sheria, Bw. Charles Mulamula, pamoja na maafisa wengine waandamizi.
Mara baada ya kuwasili, viongozi hao walipokelewa na Katibu Mtendaji wa BASATA, Dkt. Kedmon Mapana, na kufanya mazungumzo na menejimenti ya Baraza kuhusu utekelezaji wa majukumu ya watumishi na uboreshaji wa mifumo ya utendaji.
Ziara hiyo imelenga kuhakikisha taasisi za umma, ikiwemo BASATA, zinafuata kanuni, taratibu na miongozo ya Utumishi wa Umma, sambamba na kuimarisha uwajibikaji, uadilifu na ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wananchi.