Parliament Logo

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Baraza la Sanaa la Taifa

TAMU ZA SANAA ZA MAONYESHO-BASATA

12 Sep, 2025
TAMU ZA SANAA ZA MAONYESHO-BASATA


Katika kukuza na kuleta maendeleo ya Sanaa nchini,Mkurugenzi msaidizi Sanaa Za
maonyesho BASATA Bi,Lilian Shayo amezungumzia umuhimu na mchango wa Sanaa
Za maonyesho katika kuleta maendeleo nchini,Leo ijumaaa tarehe 25.07.2025

MKurugenzi msaidizi Sanaa Za maonyesho BASATA, Bi Lilian Shayo :akizungumzia
umuhimu wa Sanaa Za maonyesho na kitengo cha mawasiliano na
uhusiano.BASATA(picha na AMINA BODA)

Kwa mujibu wa Baraza la Sanaa la taifa (BASATA) lililoundwa na sheria namba 23 ya
mwaka 1984 na kufanyiwa marekebisho ya sheria namba 5 ya mwaka
2019,inaonyesha Sanaa Za maonyesho uhusika na Michezo ya kuigiza ya
jukwaani,maigizobubu,usanifu wa majukwaa,maleba,mapambo,uandishi wa
tamthiliya,ngoma na ubunifu wake,sauti na vifaa vya jukwaani,sarakasi za binadamu,
wanyama na michezo ya radio.
Akizungumza na kitengo cha mawasilino na uhusiano kwa umma BASATA Tarehe
24.07.2025 ijumaaa bi Lilian Shayo amesema kuwa Sanaa Za maonyesho zina
umuhimu mkubwa kitambulisha taifa na biasharaa
“Sanaa Za maonyesho hasa ngoma Za jadi hutumika kwa utambulisho kupitia Sanaa
hii huonyesha mtu alipotokea na utaifa wake na hukuza mnyororo wa thamani kwa
wasanii na wadau wa Sanaa kwa kuanda matamasha,hadhira na waandishii wa

habari kwa eneo husika na nchi kiujumla”
Aidha bi Lilian ameeleza zaidi kuwa Sanaa Za maonyesho hujenga Uhusiano wa
kimataifa kati ya nchi moja na nyingine kupitia matamasha mbalimbali
yanayofanywa ndani ya Afrika mashariki ikiwa ni Kenya,Uganda na Tanzania na
kuwaweka wasaniii pamoja
Ikumbukwe tu kitengo hiki cha Sanaa Za maonyesho kinafanyaaa kazi chini ya idara
ya ukuzaji na maendeleo ya sanaaa chenye jukumu la kusajili na kusimamia Sanaa
mbalimbali Za maonyesho Kama vile michezo ya jukwani,Ngoma,shairi,Ngojela na
Uandishi wa Tamthiliya

Sanaa za Maonyesho (Performing Arts)

  1. Utangulizi mfupi 
Maelezo mafupi kuhusu nafasi ya Sanaa za Maonyesho katika sekta ya sanaa
Tanzania, ikieleza kuwa ni mojawapo ya maeneo muhimu yanayosimamiwa na
BASATA chini ya Idara ya Ukuzaji na Maendeleo ya Sanaa.
Mfano:
Sanaa za Maonyesho ni miongoni mwa sekta kuu tatu za sanaa zinazoratibiwa
na BASATA, zikiwa na mchango mkubwa katika kutambulisha utamaduni wa
Kitanzania, kujenga ajira kwa wasanii, na kuimarisha uhusiano wa kimataifa
kupitia matamasha ya kisanaa.
  2. Maeneo Yanayohusika na Sanaa za Maonyesho
Orodhesha aina za sanaa zinazoangukia katika kundi hili, kama ilivyoelezwa
kwenye Sheria ya BASATA.
Mfano:
 Michezo ya kuigiza ya jukwaani
 Maigizo bubu
 Usanifu wa majukwaa
 Uchoraji na mapambo ya jukwaa
 Uandishi wa tamthiliya
 Ngoma za asili
 Sarakasi (za binadamu na wanyama)
 Uigizaji wa redio
 Ubunifu wa sauti na vifaa vya jukwaani

 3. Majukumu ya BASATA kwenye Sanaa za Maonyesho
Toa maelezo kuhusu kazi za BASATA katika kusaidia, kusimamia na kukuza
sanaa hizi.
Mfano:
 Kusajili vikundi vya sanaa za maonyesho
 Kuratibu na kutoa vibali vya matamasha
 Kuwezesha mafunzo na warsha kwa wasanii
 Kufanya tafiti kuhusu maendeleo ya sanaa
 Kushirikiana na taasisi za kimataifa kwa maendeleo ya sanaa
 4. Mchango wa Sanaa za Maonyesho kwa Taifa
Onyesha namna sanaa hizi zinavyochangia maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Mfano:
 Hutumika kama njia ya utambulisho wa kitaifa
 Huchochea uchumi kupitia matamasha na shughuli za kisanaa
 Huongeza mshikamano wa kijamii
 Hutoa ajira kwa vijana na wanawake
 Hukuza diplomasia ya kimataifa kupitia sanaa
 5. Ushirikiano wa Kimataifa
Taja baadhi ya nchi au maeneo ambayo BASATA au wasanii wa Tanzania
hushiriki matamasha ya kimataifa (mf. Kenya, Uganda n.k).
 6. Fursa kwa Wasanii
Toa mwongozo kuhusu:
 Jinsi ya kusajili kikundi cha sanaa za maonyesho
 Namna ya kuomba kibali cha onesho
 Uwezeshaji unaopatikana (mf. mafunzo, ushauri, n.k.)

Settings