Parliament Logo

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Baraza la Sanaa la Taifa

TMA kuruka kimataifa rasmi kufanyika siku mbili mf...

28 May, 2024
TMA kuruka kimataifa rasmi kufanyika siku mbili mfululizo

TMA kuruka kimataifa rasmi kufanyika siku mbili mfululizo

 

Isack Bilali, BASATA..

Kamati ya uendeshaji wa Tuzo za Muziki Tanzania (TMA) imeweka wazi na kutangaza rasmi ujio wa tuzo hizo mnamo tarehe 14 na 15 mwezi juni, 2024 ikiwa ni tofauti na miaka yote kwani hii itakua na siku mbili za ugawaji wa tuzo huku usiku wa kwanza kutakua na ugawaji wa tuzo 20 na usiku wa pili tuzo 17 na kufanya jumla ya tuzo 37 kwa siku hizo mbili.

Akizungumza na waandishi wa habari katika hoteli ya Johari Rotana jijini Dar es Salaam mjumbe wa Kamati hiyo Bi. Seven Mosha ametanabaisha kuwa kamati inafanya kazi kwa ushirikiano wa Baraza la Sanaa Taifa wanaosaidia kuratibu ambapo hadi sasa vipengele vitakavyowaniwa ni 37 huku akihamasisha wasanii kuchangamkia fursa hiyo kwakuwa kupitia TMA wataweza kujifunglia fursa kimataifa.

Aidha Bi. Mosha aliongeza kuwa, tuzo hizo za kwa mwaka 2024 zina viwango vya kimataifa kwakuwa vyombo vya Habari vya kimataifa vya BET pamoja na MTV Africa wamekuwa washirika rasmi ambapo watarusha Matangazo ya ugawaji wa tuzo hizo.

Tunayo furaha kuwatangazia wadau wote wa muziki Tanzania kwamba tuzo za muziki mwaka huu zitakua na platform kubwa yenye ubora wa kimataifa na yenye uwezo wa kutambulisha muziki wa Tanzania Dunia nzima kwani BET na MTV Africa watakua moja kati ya vyombo vya habari vitakavyorusha Matangazo na ugawaji wa tuzo za muziki za Tanzania wakiwa na lengo la kukuza, kusambaza, kuonyesha nguvu ya muziki na ubunifu kutoka Tanzania

Mashirika hayo ya utangazaji yenye nguvu na mchango mkubwa maendeleo ya sanaa Afrika na Dunia yamelenga kudhamini washindi kutoka vipengele 6 ambao watawezeshwa kuhudhuria tuzo za BET za mwaka 2024 nchini Marekani kuanzia “pre party, party na post party” zaidi ya hapo washindi hao watapata fursa ya kushirikishwa katika kutumbuiza kwenye ugawaji wa tuzo hizo za BET.

Kwa upande wa katibu wa kamati ya Tuzo hizo kutoka Baraza la Sanaa Taifa Bwana. Mrisho Mrisho ametanabaisha kuwa tuzo zinalenga kuimarisha uhusiano baina ya serikali na wadau wa sanaa kwa kukuza na kuendeleza muziki huku zikidhamiria kutangaza vivutio vya utalii vya nchini vikiwemo mbuga za wanyama, mapori tengefu, hifadhi na vivutio vingine jambo litakalofanywa kwa ushirikiano wa karibu na bodi ya utalii.

Mrisho ameongeza kuwa ili mwanamuziki aweze kushiriki na kuwania tuzo analazimika kujisajili na kuwasilisha kazi zake zilizofanyika kwa kipindi cha Januari hadi Disemba 2023, utafanyika upembuzi utakaofanywa na wataalam waliobobea katika muziki ili kupata kazi bora, kutangazwa wanaowania tuzo “Nominees”, upigaji wa kura na maamuzi ya majaji kwaajili ya kupata mshindi wa kila kipengele.

Baada ya tuzo hizo kutafanyika semina kwa vijana kutoka kwa Wasani waliofanikiwa na wadau mbali mbali wa mziki lengo likiwa ni kukuza na kuhamasisha vipaji vya vijana waliopo na wanaotaka kuingia kwenye muziki hivyo ni wakati kwa wasanii pamoja na wadau wa muziki Tanzania kushiriki kikamilifu ili kuchangamkia fursa lukuki zitakazoambatana na ushirika wa BET na MTV Africa.

Settings